Na Avelina Musa - DODOMA.
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imefanikiwa kutekeleza vipaumbele vitano muhimu vilivyolenga kuboresha ubora wa elimu, kupanua fursa za kujifunza na kuimarisha matumizi ya sayansi na teknolojia nchini.
Hayo yamesemwa na waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Adlof Mkenda wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027 ambapo amesema vipaumbele hivyo ni: Utekelezaji wa sera, mitaala na mapitio ya sheria pamoja na uandaaji wa miongozo ya utoaji elimu.
Prof.Mkenda amesema vipaumbele hivyo vimeweza Kuongeza fursa na kuimarisha mafunzo ya amali katika shule za sekondari na vyuo vya ufundi pamoja na Kuimarisha ubora wa elimu ya awali, msingi, sekondari na mafunzo ya ualimu.
"Kuimarisha uwezo wa nchi katika utafiti, ubunifu na matumizi ya sayansi na teknolojia kwa maendeleo ya uchumi wa viwanda."amesema.
Aidha,Waziri Mkenda amesema utekelezaji wa vipaumbele hivyo umeendelea kuleta matokeo chanya katika kuongeza ujuzi, kukuza ubunifu na kuandaa rasilimali watu yenye ushindani kwa mahitaji ya sasa ya soko la ajira.
.jpg)



