Na Avelina Musa - DODOMA.
SERIKALI imesema katika kuboresha huduma za hali ya hewa Tanzania TMA imekamilisha ufungaji wa mitambo miwili ya uangazi wa hali ya hewa katika viwanja vya ndege vya Mpanda na Pemba.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawe wakati akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo Bungeni Jijini Dodoma ambapo ameomba kuidhinishiwa jumla ya Sh trilioni 2.87 Kati ya fedha hizo, Sh 126,041,236,000 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Sh 2,746,696,846,000 ni fedha za Miradi ya Maendeleo.
Prof.Mbarawa amesema TMA imeendelea kuongeza Ubora wa Huduma za Hali ya Hewa kwa Kufunga Mitambo Mipya Viwanja vya Ndege vya Mpanda na Pemba.na ujenzi wa miundombinu ya hali ya hewa ikiwemo maabara ya uhakiki wa vifaa vya hali ya hewa (Calibration Center) Dar es Salaam ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 46
" Kuendelea kuboresha huduma za hali ya hewa;Serikali kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imeendelea na utoaji na udhibiti wa huduma za hali ya hewa nchini."amesema Prof.Mbarawa.
Aidha Prof.Mbarawa amesema katika Mpango na Bajeti ya mwaka wa fedha 2026/27, Wizara imezingatia Dira 2050, llani ya Uchaguzi Mkuu ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2025, Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP IV 2026/27- 2030/31), Mpango wa Taifa wa Maendeleo kwa mwaka 2026/27, Mpango Mkakati wa Wizara wa Miaka Mitano (2026/27 - 2030/31 ) pamoja na maelekezo ya Viongozi Wakuu wa Serikali.



