PROF.MBARAWA :USAFIRISHAJI KUPITIA SGR WAENDELEA KUIMARIKA

MUUNGANO   MEDIA
0

 



Na Avelina Musa - DODOMA.


Serikali imesema huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo kupitia reli ya kisasa ya SGR zimeendelea kuimarika kati ya Dar es Salaam na Dodoma, huku idadi ya wasafiri na mapato ikiongezeka kwa kiwango kikubwa.


 Hayo yamesemwa Leo Mei 13, 2026 na Waziri wa Uchukuzi,Prof.Makame Mbarawa Bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/27 ambapo amesema wastani wa abiria 280,000 husafiri kwa mwezi kupitia reli hiyo, sawa na abiria 9,300 kwa siku.


 Prof.Mbarawa amesema zaidi ya abiria milioni 3 wanatarajiwa kusafirishwa ifikapo mwisho wa mwaka wa fedha 2025/26, ikilinganishwa na wastani wa abiria 400,000 wanaosafiri kwa reli ya MGR kwa mwaka.


"Utekelezaji wa mradi huo, TRC inaendelea kutoa huduma za usafiri katika vipande vilivyokamilika, hatua inayowezesha wananchi kuanza kunufaika na maboresho ya sekta ya reli nchini."amesema.


Prof.Mbarawa amesema kwa upande wa kipande cha Mwanza hadi Isaka ujenzi umefikia asilimia 68.77 na kazi zinaendelea vizuri na hadi kufikia mwezi March mwaka huu, ujenzi wa kipande cha tatu kutoka Makutupora hadi Tabora na kipande cha nne kutoka Tabora hadi Isaka unaendelea huku shughuli mbalimbali za utekelezaji zikiendelea katika maeneo hayo.


"Kuanzia Julai 2025 hadi Machi 2026, TRC imekusanya Sh82.77 bilioni kupitia huduma za SGR, huku mapato ya jumla tangu kuanza kwa safari mwezi Juni 2024 yakifikia Sh169.37 bilioni,amesema.









Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)