Na Avelina Musa -Dodoma
Wakala wa Usajili wa biashara na leseni (BRELA)umetoa elimu ya umuhimu wa kusajili biashara na leseni ili wafanyabiashara waweze kufanya majukumu yao Kwa uhuru bila bugha yeyote.
Hayo yamesemwa Leo Jijini Dodoma na Afisa Msajili kutoka Wakala wa usajili wa biashara na Leseni (BRELA) Bwn.Gabriel Girangay wakati akizungumza katika kongamano la Elimu ya Fedha,kazi na kujitegemea kwa vijana na wanawake Kwa mwaka 2025 2025,katika ukumbi wa mikutano kwenye viwanja vya maonesho ya 88 Mkoani Dodoma.
Bwn.Girangay amesema BRELA inatoa huduma ya kusajili leseni ya biashara,Kusajili majina ya biashara,Kusajili viwanda vidogo,Usajili wa alama za biashara ambapo kusajili jina la biashara ni Tsh.20,000 ili mfanyabiashara aweze kufanya majukumu yake bila bugdha
Bwn.Girangay amesema umuhimu wa mfanyabiashara kusajili biashara ni ili itambulike na wasisumbuliwe katika biashara zao.
"Unapokuwa na vibali vyote vya Serikali,una leseni, una usajili na kila kitu na kama una kiwanda una leseni ya kiwanda hapa taasisi zote za kifedha watakuamini kupatiwa fedha, utazalisha kwa kiwango kikubwa kwa sababu utakuwa na misuli ya kifedha." Amesema Bwn.Girangay.
Akijibu swali la mshiriki wa kongamano hilo Ndg. Gabriel Samson alieuliza ni kwa namna gani BRELA inavyochangia kusaidia wakulima ambapo amesema kama mkulima unapozalisha mazao na kuyachakata utahitaji kuweka nembo ili kuyapeleka sokoni sambabmba na usajili wa leseni na jina la biashara ambao BRELA ndio wenye mamlaka ya kufanya hayo.
Aidha kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Mrutu Agro Solutions Bwana Phillips Mrutu ameeleza ushuhuda wake wa namna ambavyo BRELA imewasaidia kufanikisha malengo ya Kampuni yao na kusaidia kuaminika na Taasisi za kifedha ambazo mpaka sasa wanamahusiano mazuri na Taasisi hizo.
"Mimi ni Shuhuda kwamba tumesajili BRELA lakini katika ushirikiano na Equity Benki tulifanikiwa kuanzisha SACCOS kwa kuweka akiba kwa ajili ya wakulima,wafugaji na wajasiriamali na sasa hivi baada ya kuweka akiba tulisajii SACCOS ya wakulima na wajasiriamali ambayo tumepata leseni kutoka Benki Kuu ya Tanzania kwahiyo huu ni ushirikiano mkubwa." Amesema Mrutu.