BANK ya Equity yaingia mkataba na kampuni ya Bajaj Process Park Limited kwa ajili ya kuwainua wakulima ili kuhakikisha wanahifadhi mazao yao na kuyaongezea thamani katika soko la Kitaifa na Kimataifa na mkulima kupata faida kupitia kilimo chake hususani wakulima wa mbogamboga na matunda.
Akizungumza na waandishi wa habari tarehe 06 Agosti 2025 Bw.Shabani K. Millao Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya kondoa mara baada ya kushuhudia utiaji Saini kati ya Bajaj process park Limited pamoja na equity Bank mkataba unaohusisha Bajaj katika kusaidia kuthaminisha mazao ya wakulima.
Amesema tunaposema wakulima inamaanisha ni pamoja na mifugo kuingia mkataba na equity Bank ili kusaidia uzalishaji wa Maziwa ili yaweze kupata thamani kwani Maziwa yanapopatikana ndani ya muda mfupi na hayana sehemu sahihi ya kuhifadhia yanaweza kuharibika hivyo kupitia hawa wenzetu wa bajaj yataweza kuhifadhiwa sehemu sahihi"
"Sio Maziwa pekee hata mbogamboga na hii itamsaidia pia mkulima kwani mara nyingi anapovuna anajikuta Kwa namna moja ama nyingine mazao yanakosa thamani anauza ndani ya muda mfupi lakini Kwa Sasahivi wakulima wa parachichi wameshapata mkombozi"
"Tunaposema kuhifadhi mazao yao maana tunasema mkulima anakuwa na muda mzuri inamaana hata Bei ya mazao itaongezeka hivyo ni wasihi wakulima wanaohusika na matunda wasiwe na hofu Bali wawasiliane na watu wa Equity Bank Kwa Maelezo zaidi ya nini Cha kufanya"Amesema.
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo Cha Kilimo Biashara kutoka Equity Bank Bi.Teofola Madilu amesema wao wanajihusisha na shughuli za Kilimo na kuongeza thamani lakini pia Kwa ajili ya kupata Mikopo ambapo kikubwa katika mkataba walioingia ni mkataba uliolenga kuleta na kuongeza thamani au kupunguza hasara ya mazao.
Amesema mazao hayo yaliyolengwa ni pamoja na Maziwa na wakulima wa mbogamboga na matunda ili kupata uhifadhi wa mazao yao ili kumuwezesha mkulima kuhifadhi mazao Kwa muda ambao atautaka yeye mwenyewe na kuingia mkataba na makampuni makubwa ambayo yananunua Maziwa kama Asas na makampuni mengine.
"Maziwa yatatoka kokote na kuweza kumfikia mzalishaji mkubwa wa Maziwa kwani Kwa kufanya hivyo Kwa Kiasi kikubwa tutakuwa tumechangia ukuaji wa uchumi wa mkulima mdogomdogo lakini pia na Taifa Kwa ujumla.
Aidha amesema Tanzania Kwa Sasa ni mzalishaji mkubwa wa parachichi na anamasoko nje ya Tanzania hivyo kitu kikubwa kinachofanya wakulima washindwe kupata bei nzuri ni uhifadhi ule ubora wa Bidhaa unakuwa haupo kulingana na kiwango Cha masoko.
"Tunawakaribisha sana wananchi katika Benki yetu ya Equity wote walioko kwenye mnyororo wa thamani ya Kilimo Cha mazao lakini wote walioko kwenye Kilimo Cha mifugo kwani tuko mikoa 8 Tanzania Bara ikiwemo Dodoma,Mbeya,Morogoro,Geita,Mwanza, Kilimanjaro,Shinyanga pamoja na Arusha"
Aidha amesema pia wanafanya kazi na mashirika na taasisi za wakulima ili kuweza kuwafikia wakulima kwani Mkoa wa Ruvuma hawana tawi lakini wameweza kuwafikia zaidi ya wakulima elfu 20 kwani wana taasisi inayowasimamia ambayo inawasaidia wao kuweza kufikisha huduma kwa wakulima hivyo huduma zao zinafika kote nchini.