SIMBACHAWENE ACHUKUA FOMU KIBAKWE

MUUNGANO   MEDIA
0

 




Mtia nia  wa nafasi ya Ubunge kupitia chama cha Mapinduzi Ccm Mhe. George Simbachawene jana alifika katika ofisi za chama hicho zilizopo Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma, kwa ajili ya kuchukua fomu ya Kuomba Ridhaa ya kuwania kiti cha Ubunge katika Jimbo la Kibakwe.


Akizungumza na Waandishi wa Habari Mhe. Simbachawene amesema kuwa bado ana nafasi ya kuendelea kuwatumikia Wananchi wa Kibakwe, kwani Nguvu bado anazo na maendeleo aliyo yafanya Tangu aongoze Jimbo hilo, yameonekana kwa viwango vikubwa 


Aidha Simbachawene, amekipongeza Chama cha mapinduzi kwa kuonyesha Demokrasia ya kila Mtu mwenye Sifa kupata nafasi ya Kuwania nafasi mbalimmbali za Uongozi ndani ya Chama hicho.





Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)