Na Avelina Musa - Dodoma.
MIAKA Minne ya Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imengarisha Mkoa wa Singida kwa kuwa na ongezeka la Pato kutoka Tshs.Trilioni 2.709 mwaka 2020/21 hadi shilingi Trilioni 3.398 mwaka 2024/25.
Huku Wastani wa pato la mwananchi mmoja mmoja likitajwa kuongezeka kutoka Tshs. 1,588,604.66 (2020/21) hadi Tshs.1,710,562.00 mwaka 2024/25.
Hayo yamesemwa jijini Jijini leo Julai 4,2025 na Mkuu wa Mkoa huo Halima Dendego wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita katika Mkoa huo.
Mhe. Halima amesema makusanyo mengine yaliyoongezeka ni ya Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kutoka shilingi Bil. 11.9, 2021/22 hadi shilingi Bil.30, 2024/25 sawa na asilimia 152.
"Makusanyo ya ndani ya Madini yameongezeka kutoka shilingi Bil. 14.6 2020/21 hadi shilingi Bil. 24.8 2024/25 sawa na asilimia 69.8.
Mhe, Dendego amesema huduma za kijamii kwenye sekta ya Afya kumekuwa na ongezeko la vituo vya kutolea huduma za Afya kuanzia ngazi ya Zahanati hadi Hospitali kutoka vituo 203 mwaka 2020/21 hadi vituo 302 mwaka 2024/25 huku huduma za kibingwa tembezi na za kudumu zikiendelea kutolewa kwa wananchi.
Akizungumzia sekta ya Elimu Dendego amesema kuwa Shule mpya za msingi 142 zimejengwa,Shule mpya 40 za sekondari zimejenga,Shule mpya 7 za amali zimejengwa, Vyuo 4 vya VETA vinajengwa na kimoja kimekamilika,Takribani 48B zimetumika kutoa elimu bila malipo.
“Utoaji wa vyakula mashuleni umefikia asilimia 95 na utoro umepungua,”amesema.
Hata hivyo amezungumzia nishati ya umeme na gesi ambapo amesema uzalishaji katika kituo cha Misuna umefikia MW 616 na matumizi ya mkoa yameongezeka kutoka MW 15.19 – 21.42 sawa na asilimia 29.
Vijiji vyote 441 vimewasha umeme kwa asilimia 100 toka vijiji 243 mwaka 2021/22,Vitongoji 1,052 sawa na asilimia 46 kati ya 2,289 Vimewasha umeme na vitongoji 120 kazi inaendelea na wateja wameongezeka kutoka 74,060 2021/22 hadi 104,553 mwaka 2024//25.
“Usambazaji wa majiko ya Gesi yenye ruzuku 30,111 unaendelea na Elimu juu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia imeendelea kutolewa kwa njia ya mitandao, mikutano, makongamano na matamasha,”amesema.


