Na Avelina Musa - Dodoma.
Chama cha Mapinduzi CCM kimetangaza kuwa kesho July 26.2025 kutakuwa na mkutano Mkuu maalum wa CCM Taifa utakaotanguliwa na Vikao vya kamati kuu na Halmashauri kuu Taifa utakaoendeshwa kwa njia ya mtandao.
Hayo yamesemwa na Katibu wa Itikadi,uenezi na Mafunzo CPA Amos Makala wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma ambapo amesema agenda ya Mkutano huo Maalum ni marekebisho madogo ya katiba ya Chama cha Mapinduzi.
Amesema ajenda ya mkutano huo maalum ni moja tu ambayo ni mabadiliko madogo ya katiba ambayo yawezi kufanywa na kikao chochote zaidi ya mkutano Mkuu wa Chama
CPA Makala amesema kumekuwepo na maneno mengi kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mkutano huo unatarajiwa kufanyika kwa njia ya mtandao.
"Mabadiliko ya katiba hayawezi kufanywa na NEC,Kamati Kuu wala vikao vya Sekretarieti bali ni wenye katiba yao ambao ni mkutano mkuu",amesema CPA Makala.
Amesema kwamujibu wa katiba ya chama cha mapinduzi CCM, inawaruhusu kufanya mkutano mkuu maalum kwa njia ya mtandao pale wanapoona inafaa.
"Hadi sasa maandalizi ya mkutano huo yamekamilika na kwa mara ya kwanza watu watakwenda kushuhudi chama hicho kikifanya mkutano mkuu kwa njia ya mtandao."amesema.
Mwisho.
CPA Makala amesema Maandalizi yamekamilika kwa asilimia 100 na wilaya zipo tayari mikoa yote ipo tayari Sekretarieti tunaendelea na maandalizi ili kufanikisha mkutano huu mkuu maalum ambao utatanguliwa na vikao vya kamati kuu na halmshauri kuu ya CCM.
