SERIKALI KUONGEZA NGUVU AFUA ZA AFYA NA LISHE SHULENI.

MUUNGANO   MEDIA
0


 66.jpg
63.jpg
Bw.Victor Bwindiki, Mkurugenzi Msaidizi Sera za  Elimu Msingi kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia akizungumza katika Kikao cha Kamati ya Kitaalam cha Ushauri wa Mpango wa Taifa wa Huduma za Afya na lishe shuleni (TAC) kilichofanyika Mkoani Morogoro.


71.jpg
Dkt. Otilia Gowelle Kaimu, Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya akizungumza katika Kikao cha Kamati ya Kitaalam cha Ushauri wa Mpango wa Taifa wa Huduma za Afya na lishe shuleni (TAC) kilichofanyika Mkoani Morogoro.

32.jpg
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya  Mtoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Sebastian Kitiku akizungumza katika Kikao cha TAC kilichofanyika  mkoani Morogoro tarehe 20-21,Juni,2025.

69.jpg
Mratibu wa Mpango wa Taifa wa Afya na Lishe shuleni kutoka Wizara ya Afya Beauty Mwambebule akizungumza katika Kikao cha TAC kilichofanyika  mkoani Morogoro tarehe 20-21,Juni,2025.

 
10.jpg
Mkurugenzi wa Engender Health Moke Magoma akizungumza katika Kikao cha Kamati ya Kitaalam cha Ushauri wa Mpango wa Taifa wa Huduma za Afya na lishe shuleni (TAC).

Serikali imedhamiria kuwekeza nguvu katika eneo la lishe shuleni.

Hayo yamesemwa Mkoani Morogoro na  Mkurugenzi Msaidizi Sera za  Elimu Msingi kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia   Bw.Victor Bwindiki   wakati akifunga Kikao cha Kamati ya Kitaalam cha Ushauri wa Mpango wa Taifa wa Huduma za Afya na lishe shuleni (TAC).

"Tunashukuru sana Wizara ya Afya kwa kutukutanisha pamoja, hivyo lengo na dhamira yetu ni moja kuwa tunaongeza nguvu katika kuhakikisha Afya na lishe shuleni inaimarika ili watoto wetu wasome bila changamoto yoyote"amesema.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya Dkt. Otilia Gowelle ambaye alikuwa mwenyekiti wa Kikao hicho amesema mahali sahihi pa kuwekeza watoto ni shule hivyo kuimarisha afya na lishe ni msingi mkubwa.

"Mahali sahihi pakuwekeza watoto kuwa na afya bora ni shule hivyo ni muhimu sana lishe kutolewa shuleni kwani inamfanya kuwa na utulivu mzuri"amesema.

Wizara za Kisekta zilizokutana ni Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Rais Rais TAMISEMI, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wizara ya Elimu, Wizara ya Mifugo, Wizara ya Mifugo na Wizara ya Afya.

MWISHO.

57.jpg
45.jpg

49.jpg
38.jpg
36.jpg
13.jpg

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)