WIZARA YA KATIBA NA SHERIA YAAINISHA VIPAUMBELE VYAKE KWA MWAKA 2025/26.

MUUNGANO   MEDIA
0

 



Na Avelina Musa - Dodoma.

WIZARA ya Katiba na Sheria imeainisha vipaumbele vyake 22 ambavyo vitatekelezwa katika taasisi zake na muhimili wa Mahakama kwa mwaka wa fedha 2025/2026.


Ambapo itaendelea kuboresha utoaji wa huduma za kisheria na utoaji wa haki kwa umma ili kuendana na mipango ya Sekta ya Sheria nchini pamoja na mipango ya Kikanda na Kimataifa ili kufikia malengo yaliyopangwa kwa kipindi husika.


Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Damas Ndumbaro wakati akiwasilisha hotuba ya Wizara hiyo kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2025/2026.


Mhe.Dumbaro amevitaja vipaumbele hivyo kuwa ni kuimarisha huduma za msaada wa kisheria kwa watu wenye uhitaji na kushughulikia masuala ya kikatiba pamoja na kutoa elimu ya Katiba na Uraia kwa Umma.


Amesema kuwa kutekeleza mapendekezo ya Tume ya kuangalia jinsi ya kuboresha Taasisi za Haki Jinai Nchini, kubainisha na kutatua migogoro ya kisheria kwa wananchi na wadau wengine,kuimarisha mifumo ya utoaji haki ili haki ipatikane kwa wote na kwa wakati.


Dkt. Ndumbaro amesema vipaumbele vingine ni kuboresha mfumo wa kitaifa na kuzingatia mifumo ya kikanda na kimataifa kuhusu haki za binadamu na utawala bora, kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kimataifa katika masuala ya haki jinai na haki madai, kuwezesha matumizi ya lugha ya Kiswahili katika Sekta ya Sheria nchini.


Aidha amesema vingine ni uimarisha mifumo kisheria na kitaasisi katika Utatuzi wa Migogoro kwa Njia

Mbadala, kuimarisha usimamizi wa mikataba ya utajiri asili na maliasilia za nchi ambazo Wizara, Idara na Taasisi za Serikali zimeingia na wawekezaji, kuimarisha usimamizi,ufuatiliaji na majadiliano ya mikataba ,kuimarisha mfumo wa uandishi, ufasiri na urekebu wa sheria.


" Vipaumbele hivi ni pamoja na ujenzi na ukarabati wa miundombinu katika sekta ya sheria kusimamia na kuendeleza elimu na taaluma ya Sheria nchini, kuwezesha usajili wa matukio muhimu ya binadamu na kusimamia masuala ya ufilisi na udhamini,Amesema.


Dkt. Ndumbaro akizungumzia baadhi ya kazi zitakazotekelezwa katika Mwaka wa fedha 2025/2026 amesema katika kutekeleza vipaumbele vilivyoainishwa, baadhi ya kazi zitakazotekelezwa na Wizara ya Katiba na Sheria fungu namba 41 katika Mwaka wa Fedha 2025/2026 ni pamoja na kuandaa Sera ya Taifa ya Msaada wa kisheria,kutoa huduma za msaada wa kisheria ikiwemo kutekeleza kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia.


"Kuimarisha mfumo wa usimamizi, uratibu na kuwajengea uwezo wataalam wa Utatuzi wa Migogoro kwa Njia Mbadala, kuratibu na kuwezesha Mapitio ya Sheria zinazohusu Haki jinai,kuwezesha uandaaji wa miongozo ya ufuatiliaji wa masuala ya haki za binadamu pamoja na uandishi wa taarifa za Haki za Binadamu,Amesema.


Mwisho

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)