WAKAZI WA DODOMA NA MIKOA JIRANI WAITWA KATIKA MAADHIMISHO WIKI YA AFYA 2025

MUUNGANO   MEDIA
0

 




Na Avelina Musa - Dodoma.

Wakazi wa Dodoma na Mikoa jirani Waitwa katika maadhimisho  ya wiki ya Afya 2025 yanayoendelea Jijini hapa katika viwanja vya Jakaya Kikwete Convetion ambapo wameaswa kujitokeza  kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa magonjwa mbalimbali.
Wakizungumza leo Aprili 5,2025 baadhi ya wananchi waliopata huduma wameishukuru serikali kwa kuwaletea huduma bobezi karibu bila malipo. 
Neema Isaya Mkazi wa Miyuji amesema anaishukuru wizara ya afya kwa kuleta huduma ya afya bila gharama ambapo anasema amehudumiwa vizur na amepima macho na ngozi.
"Yaani serikali imetusaidia sana ukienda hospital hizi huduma tunalipia lakini hapa ni Bure na nikitoka hapa naenda Banda lile linalopima saratani ya mlango wa kizazi ili nijue Niko salama"Amesema Neema.


"Wakazi wa Dodoma hii fursa tusiichezee tujitokeze kujua afya zetu"Amesema Neema.
 Naye Emmanuel Masawe  Mkazi wa Dodoma Makulu ameishukuru serikali kwa utoaji wa huduma hizo ambapo ameiomba wizara ya Afya kuifanya huduma hiyo iwe endelevu kwa sababu hospitalini ni gharama.
“Tunatamani Sana Kila Mtanzania aweze kufikia Jakaya Kikwete kupata huduma rafiki na nzuri hapa tunapima magonjwa yote,”amesema Bw.Masawe
Aidha Kwa Upande wake Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Afya ya akili,Dkt.Veronica Lymo amesema katika wiki ya Afya 2025 wamejiandaa kutoa huduma kwa watanzania wote.

Dkt.Veronika amesema wapo katika wiki hiyo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa awali kwa watu wote na iwapo watagundulika wana changamoto watahakikisha wanapata tiba sahihi.
Amesema Hospitali ya Mirembe inahusika na magonjwa ya akili na changamoto ya afya ya akili huku akidai wanahudumia wagonjwa wote wa magonjwa ya ndani.
Kwa upande wake Dk Abasi Msaji kutoka Hospitali amesema wanatoa huduma za upimaji wa sukari,pressure,ushauri kuhusu uzito.

Maadhimisho ya Wiki ya Afya kitaifa yaliyoanza tarehe 3 - 8, Mwezi 4, 2025 Katika Viwanja vya  CCM Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma ambapo huduma mbalimbali za Upimaji na Uchunguzi wa awali zinapatikana  ambazo ni

1. Upimaji wa Figo

2. ⁠Upimaji wa Magonjwa ya Moyo na Mishipa

3. ⁠Upimaji wa Shinikizo la Damu  (BP)

4. ⁠Upimaji wa Ugonjwa wa Kisukari

5. ⁠Upimaji wa Kifua Kikuu

6. ⁠Upimaji wa Uzito na hali ya lishe

7. ⁠Huduma za Kinywa na Meno

8. ⁠Upimaji na matibabu ya Macho

9. ⁠Huduma za uzazi wa Mpango

10. ⁠Upimaji wa Saratani ya Matiti na Mlango wa Kizazi.

11. ⁠Chanjo ya Saratani ya Mlango wa kizazi (HPV)

12. ⁠Msaada wa saikolojia na Afya ya Akili

13. ⁠Elimu ya Lishe

14. ⁠Upimaji wa Saratani

Huduma hizi zinatolewa na  Watalaamu Bingwa na Bobezi kutoka katika Hospitali za *JKCI, BUGANDO, BENJAMINI MKAPA, UDOM, DODOMA GENERAL HOSPITAL, KIBONG'OTO HOSPITAL, OCEAN ROAD, KCMC, MIREMBE NA MOI*

Muda ni kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni na huduma zote zinatolewa bila malipo na Wiki ya Afya Kitaifa inakwenda sambamba na kaulimbiu isemayo"Tulipotoka, Tulipo, Tunapokwenda, Tunajenga Taifa Imara lenye Afya.

MWISHO.

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)