MHE.SIMBACHAWENE AELEZA MAFANIKIO LUKUKI NDANI YA MIAKA MINNE YA RAIS MHE.DKT.SAMIA.

MUUNGANO   MEDIA
0

 





Na Avelina Musa - Dodoma.


Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mhe.George Simbachawene amesema Katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita Taasisi 275 katika Utumishi wa Umma zimejengewa uwezo kuhusu uzingatiaji wa  Sheria,  Kanuni  na  Taratibu kwenye  ushughulikiaji  wa  masuala  ya Kiutumishi.


Mhe,Simbachawene amesema hayo Leo  Aprili 17,2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea mafanikio na mwelekeo wa Wizara hiyo katika kipindi Cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita  Jijini Dodoma.


"Taasisi 543 zilikaguliwa kwa lengo la kuangalia uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu zinazosimamia masuala ya Kiutumishi"Amesema Simbachawene.


Amesema ukaguzi huo umesaidia kukua kwa kiwango cha uadilifu kwa watumishi wa umma kama ilivyobainishwa kupitia utafiti uliofanywa na Ofisi mwaka 2022 kuhusu hali ya uadilifu katika utumishi wa umma, ambapo utafiti ulibainisha kuwepo kwa ongezeko la 9.8% kutoka 66.1% (2014) hadi 75.9% (2022);

Katika kipindi cha kuanzia Mwaka 2020 hadi Mwezi Agosti, 2024, Ofisi imefanya uhamasishaji wa Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma kwa taasisi za Umma 88 kwa jumla ya Watumishi 3,443 kutoka katika Mikoa ya Mbeya, Mtwara, Mwanza Arusha na Kilimanjaro. 

"Ofisi imeendelea kushirikiana na Taasisi Simamizi za Maadili kwa kuzijengea uwezo Kamati za Uadilifu kupitia Mkakati wa Taifa Dhidi ya Rushwa na Mpango wa Utekelezaji kwa awamu ya III na sasa ya IV, ambapo katika kipindi cha Kuanzia Mwaka 2020 hadi Mwezi Agosti, 2024 Ofisi imezijengea uwezo Kamati za Uadilifu 59 zenye jumla ya watumishi (Wajumbe) 700 kwa njia ya  mafunzo ya Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma ikiwa ni sehemu ya kuimarisha nidhamu, utendaji kazi na uwajibikaji"Amesema Simbachawene.

Amesema utaratibu huo umeleta mafanikio makubwa ambapo uwajibikaji umeongezeka kwasababu ya urahisi wa ufuatiliaji kupitia mifumo ya TEHAMA, na wananchi wameongeza imani yao kwa Serikali kutokana na namna wanavyohudumiwa na kupata mrejesho kwa njia rafiki zinazowapunguzia gharama za usafiri kwa ajili ya ufuatiliaji;.

Aidha amesema Katika kupambana na upungufu wa ajira, Serikali kupitia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ilifanikisha mchakato wa Ajira na kuwapangia vituo vya kazi jumla ya waombaji wa kazi 55,162 ambapo waombaji kazi waliopangiwa vituo vya kazi waliongezeka kutoka 7,659 mwaka 2020 hadi 20,158 mwaka 2024, sawa na ongezeko la asilimia 163.19.

"Serikali kupitia Ofisi hii baada ya kuona kuna tatizo la upungufu wa watumishi katika maeneo mengi, ilitafuta namna bora ya kuondoa changamoto hiyo kwa kujenga Mfumo wa Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu (HR-Assessment). Mfumo huu wa Tathmini ya Mahitaji ya Rasilimaliwatu ni msaada mkubwa kwani unabainisha idadi ya watumishi walioko katika kila kituo cha kazi na upungufu au ziada iliyopo ili kuwa na idadi ya watumishi sahihi katika sehemu sahihi za utekelezaji wa majukumu yao"Amesema.




Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)