Na Avelina Musa - Dodoma.
Akizungumza na waandishi wa habari Leo April 30.2025 Jijini Dodoma Kiongozi wa Sifa na Ibada Tanzania Mtumishi Elia Mwantondo amesema Sasa ni zamu ya Dodoma kupata baraka hizi kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Mwantondo amesema Dodoma ni makao makuu ya Nchi hivyo ni vyema kuwa na Ibada ya kuiombea Taifa hasa katika mwaka huu ili Nchi iwe na Amani na Utulivu.
"Kama Nchi tunapaswa kuwa na Ibada ya kumtukuza Mungu na maombi ya kuiombea Taifa ili tuwe salama maana hata Neno la Mungu Linasema heri Taifa ambalo Bwana ndio Mungu wao"Amesema Mwantondo.
Ibada hiyo inatarajiwa kufanyika kesho Mei Mosi 2025 katika Ukumbi wa Mabeho Jijini Dodoma kuanzia saa nane mchana ambapo waimbaji mbali mbali watakuwepo.
Kwa Upande wake Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Sara Ndosi amesema umefika muda wa wanawake na mabinti kurudi katika nafasi Yao ya kuomba na kumtukuza Mungu.
Naye Mwimbaji Ambwene Mwasongwe amewasihi wakazi wa Dodoma kujitokeza kwa wingi katika Ibada hiyo yenye lengo la kumsifu na kumwomba Mungu.
Mwisho.