UCSAF YATOA MAFUNZO YA TEHAMA KWA WALIMU 1,585 KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MINNE YA SERIKALI YA AWAMU YA SITA.

MUUNGANO   MEDIA
0

 





Na Avelina Musa - Dodoma.

Katika kipindi cha Miaka Minne ya Serikali ya Awamu ya Sita,Mfuko wa mawasiliano kwa wote(UCSAF) umetoa mafunzo ya Tehama kwa  Walimu 1,585 Nchini.

Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo walimu kutatua matatizo ya vifaa vya Tehama na kuwafundisha wanafunzi kwa weledi.

Hayo yameelezwa na Afisa Mtendaji Mkuu, Mfuko wa mawasiliano kwa wote(UCSAF) Mhandisi Peter Mwasalyanda leo Jijini Dodoma  wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya miaka minne ya serikali ya awamu ya sita. 


Mhandisi Mwasalyanda amesema mafunzo ya TEHAMA yametolewa katika shule 1791 ambapo Zanzibar walimu 326 na Tanzania Bara walimu 3,180 lengo likiwa ni kuwajengea uwezo walimu kutatua matatizo ya vifaa vya TEHAMA.




"Elimu hiyo kwa walimu itawawezesha kuvielewa vifaa vya TEHAMA hata pale vinaposumbua wasipate usumbufu wa kuwatafuta mafundi kwa mambo ambayo wanaweza kuyafanya wenyewe na kuwafundisha wanafunzi kwa uelewa zaidi"Amesema Mhandisi Peter.


Aidha amesema UCSAF imeingia mikataba ya kufikisha mawasiliano katika kata 1,974 zenye vijiji 5,102 vyenye wakazi 29,193,753 ambapo inajengwa jumla ya minara 2,152. Kati ya miradi hiyo, jumla ya minara 1,783 imekamilika katika kata 1,627 zenye vijiji 4,482 vyenye wakazi 24,640,304. 

"Hadi kufikia march 24.2025, minara 430 kati ya minara 758 imejengwa na kuanza kutoa huduma kwa wananchi wa maeneo ya vijiji"Amesema Mhandisi.

Amesema Ruzuku ya shilingi bilioni 5.51 imetumika kwa ajili ya kuboresha uwezo wa minara ambapo jumla ya minara 304 imeongezwa nguvu kutoka 2g kwenda 3g/4g.

Hata hivyo kwa Upande wake, Katibu Mkuu  Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa amesema Serikali imefanya kazi kubwa katika kipindi cha miaka minne ambapo utendaji huo umetokana na nia, maono na msimamo alionao Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

"Nawashukuru Waandishi wa Habari kwa sababu kupitia mfululizo wa mikutano hii, Watanzania wamesikia utekelezaji wa taasisi za umma 35"Amesema Bw.Msigwa.

Mwisho.


Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)