Na Avelina Musa - Dodoma.
Shirika la viwango Tanzania (TBS) limetenga kiasi cha Sh. Bilioni 2.7 kwa ajili ya kuimarisha ofisi saba za kanda ili kusogeza huduma kwa wananchi.
Ofisi hizo zinatarajiwa kujengwa katika Mikoa ya Arusha, Mwanza, Mtwara, Dar es Salaam, Dodoma, Kigoma na Mbeya) pamoja na ofisi za mipakani (Tunduma, Kasumulo, Horohoro na Holili.
Hayo yameelezwa leo march 18/2025 Jijini Dodoma na Mkurugenzi Mkuu wa TBS Dkt. Ashura Katunzi, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa shirika hilo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita.
"Ofisi nyingine ni Tarakea, Namanga, Bandari ya Mwanza, Uwanja wa Ndege wa Mwanza, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, Sirari, Kabanga, Rusumo, Mutukula, Bandari ya Bagamoyo, bandari ya Mbweni, bandari ya Dar es Salaam, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere – Dar es Salaam na Bandari ya Tanga)"Alisema Dkt.Katunzi.
Aidha Dkt. Katunzi amesema kwa upande wa Dodoma, maabara zitakazojengwa zitahudumia mikoa mitatu ya Kanda ya Kati ambayo ni Dodoma, Singida na Tabora pamoja na mikoa mingine ya karibu.
Aidha,amesema maabara za Mwanza zinatarajiwa kuhudumia mikoa sita, ambayo ni Mwanza, Kagera, Mara, Geita, Shinyanga na Simiyu.
Dkt. Katunzi amesema hatua hiyo ya ujenzi wa maabara itasaidia kusogeza huduma karibu na wananchi na kuongeza ufanisi katika utoaji wa majibu ya vipimo vya sampuli.
Amesema kuwa fedha hizo pia zitatumika kuongeza wafanyakazi na vitendea kazi kwa ajili ya kutoa huduma kwa wakati na kuimarisha zoezi la ukaguzi wa mara kwa mara sokoni ili kupunguza bidhaa hafifu sokoni na hatimaye kuhakikisha wananchi wanapata bidhaa bora na salama.
mwisho.