NSSF YAFANIKIWA KUANDIKISHA WANACHAMA 1,052,176 KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 4.

MUUNGANO   MEDIA
0

 


Na Avelina Musa - Dodoma.


Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeongeza uwezo wa kukusanya michango ambapo jumla ya Shilingi Bilioni 6,994.52 zimekusanywa kutoka kwa wanachama na michango inayokusanywa kwa mwaka ikiongezeka kutoka Shilingi bilioni 1,131.92 Februari 2021 hadi Shilingi Bilioni 2,153.13 Februari 2025 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 90.


 Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)Bw. Masha Mshomba leo Jijini Dodoma Machi 17,2025 wakati akizungumza na Wanahabari akielezea mafanikio na mwelekeo wa Mfuko huo kuelekea Maadhimisho ya miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita. 


"Katika kipindi cha miaka minne Mfuko umeongeza uwezo wa kukusanya michango ambapo jumla ya Shilingi Bilioni 6,994.52 zimekusanywa kutokabkwa kwa wanachama na michango inayokusanywa kwa mwaka ikiongezeka kutoka Bilioni 1,131.92 katika mwaka ulioishia Februari 2021 hadi kufikia Shilingi Bilioni 2,153.13 katika kipindi kilichoishia Februari 2025 sawa na ongezeko la asilimia 90".


Mshomba amesema katika kipindi cha miaka minne thamani ya vitega Uchumi vya mfuko imeongezeka kutoka Bilioni 4,283.32 katika mwaka ulioishia Februari 2021 hadi kufikia Shilingi bilioni 8,212.92 katika mwaka mwaka ulioishia Februari 2025 sawa na asilimia 92.


Aidha,Mshomba amesema ustahimilivu wa Mfuko umetokana na tathmini ya uhai na uendelevu wa Mfuko kuwa imefikia asilimia 90.7 ambapo matokeo yameonesha katika kipindi kinachoishia Juni 2023 kiwango cha sasa cha uchangiaji cha asilimia 20 kinatosha kugharamia ulipaji wa mafao,gharama za uendeshaji pamoja na gharama zingine kwa kipindi kirefu.


Mshomba amesema uandikishwaji wa wanachama wapya wapatao 1,052,176 katika kipindi cha miaka minne kinachoanzia Machi 2021 mpaka Februari 2025 ambapo Serikali ya awamu ya sita imetekeleza mikakati mbalimbali katika kuimarisha uchumi na kufungua fursa za uwekezaji na Biashara katika kipindi hicho.


NSSF imepewa dhamana ya kutoa huduma ya Hifadhi ya Jamii kwa wafanyakazi wa serikali na sekta binafsi na wananchi waliojiajiri kwa mujibu wa Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Sura ya 50.


Mwisho

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)