Na Avelina Musa - Dodoma.
KATIKA Kipindi cha Miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassani,Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) imefanikiwa kuanzisha huduma mpya za kibobezi ,Upanuzi wa Miundombinu na upatikanaji wa Vifaa tiba.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba na mifupa ya Ubongo(MOI) Dkt.Mpoki Ulisubisya wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma kuelekea maadhimisho ya miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita, kuhusu mafanikio na mwelekeo wake.
"Katika kipindi hiki cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, MOI imefanikisha kuanzisha na kuendeleza mambo mbalimbali kama vile:- Kuanzisha huduma mpya za kibobeziUpanuzi wa miundombinu Upatikanaji wa vifaa tiba Mafunzo na Kupandishwa madaraja watumishi"
Dkt.Mpoki amesema huduma nyingine iliyoboreshwa ni pamoja na Upasuaji wa Nyonga na magoti wa marudio wagonjwa 74 Wamehudumiwa Upasuaji wa mgongo kwa njia ya matundu wagonjwa 17 wamefanyiwa Matibabu ya kiharusi kwa kupitia mishipa mikubwa ya damu ya paja wagonjwa 41 wamehudumiwa.
Amesema katika kipindi cha miaka minne kuanzia mwaka 2021, Taasisi ya Mifupa MOI imehudumia jumla ya wagonjwa 816,383 kama wagonjwa wa nje na wale wa dharura (OPD na EMD), ambapo kumekuwa na wastani wa ongezeko la wagonjwa 3,023 kwa mwaka.
Kwa upande wa wagonjwa wa ndani (IPD), jumla ya 35,170 walihudumiwa, ikiwa ni wastani wa ongezeko la wagonjwa 453 kila mwaka,aidha, wagonjwa 30,289 walifanyiwa upasuaji, ambao ni sawa na 86.2% ya wagonjwa waliolazwa.
Pia, Taasisi ya MOI imeendelea kutoa huduma nyingine za kibingwa Bobezi na kupunguza rufaa za kupeleka wagonjwa nje ya nchi kama Upandikizaji wa nyonga bandia wagonjwa 728 wamehudumiwaUpandikizaji wa goti bandia wagonjwa 636 wamehudumiwaUpasuaji wa magoti kwa njia ya matundu wagonjwa 1,115 wamehudumiwaUpasuaji wa kuondoa vivimbe vya mishipa ya damu kwenye ubongo (Aneurysm) 14 wamehudumiwa
"Upasuaji wa mfupa wa kiuno wagonjwa 395 wamehudumiwa Upasuaji wa kichwa kikubwa na mgongo wazi watoto 1,797 wamehudumiwa Upasuaji wa ubongo kwa kufungua fuvu 815 Upasuaji wa mgongo wagonjwa 1,061 wamehudumiwa"
Aidha Katika kipindi cha miaka minne, Taasisi ya MOI imefanikiwa kutoa huduma za kibobezi kwa wagonjwa 7,366 ambapo gharama za matibabu haya ndani ya nchi zilikuwa Shilingi za Kitanzania bilioni 68,451,603,600.00 na kama wagonjwa hawa wangepelekwa nje ya nchi kwa matibabu jumla ya shilingi bilioni 218,280,169,470 zingetumika,hivyo serikali imefanikiwa kuokoa shilingi bilioni 149,828,565,870.00 ambazo zimetumika katika shughuli nyingine za maendeleo.
Mwisho.