MIAKA MINNE YA RAIS DKT. SAMIA MAABARA YA MKEMIA MKUU YAPATA MAFANIKO LUKUKI.

MUUNGANO   MEDIA
0

 



Na Avelina Musa - Dodoma.


Katika Miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), imefanikiwa kuendelea kutoa huduma za Uchunguzi wa Kimaabara kwa Viwango vya Kimataifa na kupata Ithibati ya umahiri wa uchunguzi wa kisayansi katika maabara zake.


 Kauli hiyo imetolewa Jijini Dodoma na Mkemia Mkuu wa serikali Dk Fidelice Mafumiko wakati akielezea mafanikio na matarajio ya mamalaka hiyo katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt. Samia ambapo amesema GCLA imepata mafanikio makubwa.


Amesema Maabara hiyo Kwa Sasa inao uwezo wa kupokea na kufanya uchunguzi wa sampuli na kutoa matokeo yanayokubalika kitaifa na kimataifa.


Dkt. Fidelice amesema mafanikio hayo yametokana na juhudi za mhe.Rais na utendaji wake wa kidiplomasia ambapo umesaidia Mamlaka hiyo kutekeleza mifumo miwili ya ubora na umahiri ya kimataifa, ambayo ni Ithibati ya Mifumo ya Usimamizi wa Ubora (ISO 9001:2015).


Dk.Fidelice amesema katika miaka minne Serikali ya Dkt. Samia imefanya uwekezaji katika mitambo na vifaa vya kisasa vya uchunguzi kwa ajili ya kuendelea kuboresha huduma za uchunguzi wa kisayansi wa kimaabara.


"Mitambo na vifaa hivi ni pamoja na mitambo mikubwa 16 na midogo 274 yenye thamani ya jumla ya Shilingi Bilioni 17.8. Ununuzi wa mitambo hii umeendelea kuimarisha uchunguzi wa kimaabara na kuendelea kutoa huduma bora za uchunguzi wa Kisayansi wa kimaabara kwa wananchi kwa ufanisi zaidi," amesema.



Aidha,Dkt.Fidelice amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia uchunguzi wa Kisayansi wa kimaabara kwa sampuli,vielelezo umeongezeka kutoka sampuli 155,817 Mwaka fedha 2021/2022 hadi kufikia sampuli 188,362 kwa mwaka wa fedha 2023/2024, sawa na ongezeko la asilimia 21.


Hata hivyo Dkt.Fidelice ameeleza matarajio ya mamlaka hiyo kuwa inatarajia kuendelea kuimarisha huduma za Uchunguzi wa Kisayansi wa kimaabara kwa sampuli na utoaji matokeo ya uchunguzi kwa wakati.


Mwisho.

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)