WATAALAMU KUTOKA WIZARA YA AFYA WAKUTANA MKOANI MOROGORO KUANDAA NA KUPITIA VIELELEZO VYA KUELIMISHA JAMII KUHUSU KUJIKINGA NA UGONJWA WA TRAKOMA NA USUBI.

MUUNGANO   MEDIA
0

 


Na. Elimu ya Afya kwa Umma.


Wataalamu wa Maudhui , Wachoraji wa vibonzo, Wasanifu, na Wataalamu wa Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele kutoka Wizara ya Afya leo tarehe 12, Agosti, 2024 wamekutana Mkoani Morogoro katika Kikao cha kuandaa vielelezo vya kuelimisha Jamii kuhusu Kujikinga na Ugonjwa wa Trakoma na Usubi.


Katika Kikao hicho ,Wizara ya Afya, kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele kwa Kushirikiana na Wadau wa Save the Children na Act to END NTDs East inaandaa vielelezo vya kuelimisha jamii ili iweze kujikinga na Magonjwa hayo kwa kushiriki kwenye afua za kumeza Kingatiba kila zinapotolewa kwenye jamii .


Hatua zingine ni kuwa na desturi ya kunawa mikono mara kwa mara, kujenga choo bora na kukitumia, kunawa mikono kila baada ya kutoka chooni, usafi binafsi na usafi wa mazingira.


Ikumbukwe kuwa kikao hicho kinafanyika kwa siku 5 kuanzia leo tarehe 12 hadi 16, Agosti, 2024.


MWISHO.

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)