TUME YA NGUVU ZA ATOM TANZANIA YALENGA KUWASAIDIA WAKULIMA NA WAFUGAJI KUFANYA SHUGHULI ZAO KWA TIJA.

MUUNGANO   MEDIA
0


Na Avelina Musa - Dodoma.

Tume ya Nguvu za Atom Tanzania imeendelea kushughulika na masuala ya uhamasishaji wa matumizi ya Nuclear nchini kwa usalama na katika jukumu hilo wamelenga kuhakikisha teknolojia ya nuclear nchini inatumika vizuri na inakuza uchumi wa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Kanda ya kati Tume ya nguvu za Atom Tanzania Machibya Anthony Matulanya kwenye maonesho ya Kitaifa ya wakulima Nanenane wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma.

Machibya amesema Tume hiyo imelenga kumsaidia mkulima na mfugaji kupata mavuno makubwa na yenye tija.

Aidha Matulanya amesema teknolojia ya Nuclear imehusika pia katika kilimo kuzingatia ukame, uzalishaji, uhimilifu wa mmea pamoja na utamu wa bidhaa baada ya mavuno.

Hata hivyo amewataka watanzania kufika kwenye banda la Tume ya nguvu za Atom Tanzania ili kushuhudia na kupata elimu ya matumizi ya mbegu ambayo inalenga kumkomboa mkulima kiuchumi.

MWISHO…

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)