MAKUNDI YA KIJAMII YAFANYIWA DODOSO KUHUSU MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE.

MUUNGANO   MEDIA
0

 



Leo Agosti 15, 2024 Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele chini ya Wizara ya Wizara ya Afya ikishirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI wameendelea na Kikao cha kuandaa vielelezo vya kuelimisha Jamii kuhusu Kujikinga na Ugonjwa wa Trakoma na Usubi ikiwa leo ni Siku ya nne.


Katika Kikao hicho ,Wizara ya Afya, kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele pamoja Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa Kushirikiana na Wadau wa Save the Children -Act to END NTDs East inaandaa vielelezo vya kuelimisha jamii ili iweze kujikinga na Magonjwa hayo kwa kushiriki kwenye afua za kumeza Kingatiba kila zinapotolewa kwenye jamii .


Afua zingine ni kuwa na desturi ya kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni, kujenga choo bora na kukitumia, usafi binafsi na usafi wa mazingira.


 Wataalamu wa Maudhui na Wasanifu wa Picha wamejadili kuhusu vielelezo vya Mitandao ya Kijamii .


Halikadhalika makundi ya Kijamii wakiwemo baadhi ya viongozi Serikali za mitaa, Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii na baadhi ya wananchi wengine wamefanyiwa dodoso kwa kuhojiwa namna walivyo na uelewa kuhusu Magonjwa yaliyokuwa hayapewi Kipaumbele, nini kifanyike katika kukabiliana nayo?


Ikumbukwe kuwa kikao hicho kinafanyika kwa siku 5 kuanzia tarehe 12 hadi 16, Agosti, 2024.


#UsibakiNyuma #MtuNiAfya


Fanya kweli Usibaki nyuma,Mtu ni Afya.


Kwa taarifa,Elimu na Ushauri zaidi Piga Simu 199

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)