Na Avelina Musa - Dodoma.
Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo(LGTI) pamoja na Campas zake Kimejipanga kuanza kutoa mafunzo kwa njia ya mtandao Kwa program ya Cheti mpaka Degree kwa mwaka wa masomo 2025/26.
Mfumo huo wa mafunzo kwa njia ya mtandao utasaidia kuboresha upatikanaji wa Elimu na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma ambapo utawasaidia wanafunzi kupata ujuzi na maarifa yanayoendana na soko la Ajira.
Hayo yameelezwa leo Agosti 7,2024 Jijini Dodoma na Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma,tafiti na Ushauri wa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Professa Magreth Bushesha wakati akizungumza na waandishi wa habari mara alipotembelea Banda la chuo hicho katika maonesho ya kitaifa ya wakulima-Nanenane (88) Nzuguni
Prof. Bushesha amesema kwa mwaka wa masomo 2025/26 chuo hicho na Kampasi zake zote kitaanza kutoa mafunzo kwa njia ya mtandao kwa program za cheti mpaka Degree ambapo kwa sasa wanatoa mafunzo hayo mtandaoni kwa kozi za muda mfupi .
" LGTI imejipambanua kujiendesha kidigili ambapo katika kozi fupi tunazozitoa zimechangia kwa kiasi kikubwa kuboresha utendaji kazi kwenye sekta ya serikali za mitaa"alisema Prof.Bushesha .
" Tumefarijika kuona watendaji wetu sasa wanavyoziangalia changamoto na kuzifanya kuwa fursa ,kupitia masomo yanayotolewa Chuoni kwetu changamoto mbalimbali zinatatuliwa kwa weledi ,kabla serikali haijatia mkono wake ,ni jambo la kujivunia,"amesema Prof Bushesha .
Aidha,Maonesho ya Kimataifa ya nane nane mwaka huu yamebeba kauli mbiu "Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa Kwa Maendeleo Endelevu ya kilimo,Mifugo na Uvuvi".
Mwisho.