Katika utekelezaji wa kampeni ya mtu
ni afya,wito umetolewa kwa wakazi wa jiji la dodoma kujenga tabia ya kufanya
usafi mara kwa mara katika maeneo yanayowazunguka ili kujikinga na magonjwa ya
mlipuko.
Wito huo umetolewa Jijini Dodoma na
Mkuu wa Kitengo cha Usafi na Mazingira Halmashauri ya Jiji la Dodoma Dickson
Kimaro wakati wa zoezi la Uhamasishaji kufanya usafi katika jiji hilo.
Mwenyekiti wa vikundi vya Usafi
Halmashauri ya Jiji la Dodoma Seleman Sanya amesema ni muhimu kuzingatia
usafi wa mita tano kila upande katika mazingira yanayokuzunguka.
Nao baadhi ya wananchi Jijini Dodoma
akiwemo Anna Jonas wamesema wameitikia wito wa kufanya usafi katika kuyaweka
mazingira katika hali ya usafi ili kuzuia vimelea vya magonjwa.