JESHI LA POLISI LAPONGEZWA KWA KUDHIBITI UHALIFU

MUUNGANO   MEDIA
0


 


Mchungaji Benjamin Bukuku wa kanisa la TAG amevipongeza vyombo vya ulinzi na usalama nchini hususani Jeshi la Polisi kwa namna ambavyo linaendelea kushirikiana na viongozi wa dini katika kuelimisha wananchi kuhusu madhara ya vitendo vya uhalifu pamoja na umuhimu wa kutunza amani ya taifa.

Mchungaji Bukuku ameyasema hayo wakati wa hafla ya uvishaji wa nishani iliyofanyika katika shule ya Polisi Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali kutoka Kanda ya Kaskazini  inayohusisha mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara.

 

Kwa upande wake kiongozi wa kanisa Katoliki lililopo katika Shule ya Polisi Moshi Padri Daniel Amani amewapongeza waliotunukiwa nishani na kuwaasa waende wakatimize majukumu yao kwa misingi ya sheria na kutii maagizo yanayotolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi.

Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura amewataka Makamanda wa Polisi pamoja na askari waliotunukiwa nishani hizo Kwenda kufanya kazi kwa kuzidisha tija na kuhakikisha nchi inaendelea kuwa salama kwa kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao na kuwahudumia wananchi kwa kutoa huduma bora na kupunguza malalamiko kutoka kwa wananchi.


Naye mkuu wa Shuke ya Polisi Moshi SACP Ramadhani Mungi akiwawakilisha wenzie aliotunukiwa nao nishani na Mkuu wa Jeshi la Polisi kwa niaba ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amesema watahakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa nidhamu, weledi na uadilifu na kutoa huduma bora kwa wananchi


CUTS ZIPO MWISHO


Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)