WATENDAJI WAZEMBE TANESCO KUANZA KUCHUKULIWA HATUA KILA MWEZI - DKT. BITEKO

MUUNGANO   MEDIA
0


 Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko ameagiza

ripoti  ya taarifa kila wiki ya Kituo cha Huduma kwa Wateja ya
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ianze  kutolewa kila mwezi ili
kufahamu maeneo yenye changamoto ya umeme nchini na kurahisisha
watendaji wazembe kuchukuliwa hatua kwenye maeneo hayo.



Dkt. Biteko ametoa agizo hilo wakati wa ziara kwenye kituo hicho cha
huduma kwa wateja leo tarehe 4 Aprili, 2024 jijini Dar es Salaam na
kutoa maagizo mbalimbali yenye lengo la kuongeza ufanisi wa kituo
hicho muhimu kwa wananchi nchini.



"Wateja wote wanaopiga simu kwa sababu mnaletewa matatizo ya wananchi
ni lazima mtengeneze kila wiki tupate  ripoti ni mkoa gani
wanahudumiwa wateja kwa haraka na mkoa upi haupewi huduma kwa haraka
ili tuchukue hatua," amesisitiza Dkt. Biteko.



Ameagiza kila mkoa nchini uliopo chini ya TANESCO ufanyiwe tathmini
kujua umeme umekatika mara ngapi na kufahamu sababu zilizopelekea
umeme kukatika katika maeneo hayo ili kama ni uzembe umefanyika
Serikali iweze kuchukua hatua haraka.



"Mimi ninafahamu kuna wakati umeme unakatika sio kwa sababu ya
matatizo makubwa bali ni kwa matatizo madogo madogo ya kiusimamizi
kwenye laini zetu. Unakuta kuna mahali mti umedondoka kwenye njia zetu
na unachukua muda mrefu kuondolewa, au mteja amepiga simu anachukua
muda kuhudumiwa, tunahitaji hiyo ripoti," amesisitiza Dkt. Biteko.



Katika hatua nyingine Dkt. Biteko ameagiza, kituo kuangalia utaratibu
wa namna nzuri ya wateja kutogharamia malipo kipindi wanapopiga simu
kuhudumiwa na kituo.



"Kiu yangu ni kuona kwamba tunakuwa na mfumo wa kupiga simu kwa Wateja
bila ya kuwaingiza kwenye gharama kwa sababu kuwaingiza kwenye gharama
haina maana yoyote kwa wanachi," ameongeza Dkt. Biteko.



Dkt. Biteko amemuagiza Meneja wa Kituo hicho kuhakikisha taarifa ya
Maendeleo ya kituo hicho kwa kila mkoa inawasilishwa  kwa Katibu Mkuu
Wizara ya Nishati ili kuongeza ufanisi wa watendaji nchini na
asipofanya hivyo atafanyiwa  mabadiliko katika kipindi cha miezi
mitatu kuanzia sasa.



Vile vile, ameagiza TANESCO kuhakikisha inajenga taswira nzuri ya nchi
kupitia watendaji wa Shirika hilo kupitia kituo hicho. Amesema fedha
zilizotolewa na Serikali za dharura kiasi cha shilingi bilioni 2.9
watu wahudumiwe ili kufurahia kuwa Watanzania kwa kupata huduma bora

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)