Maandalizi ya Timu 8 zitakazoshiriki kuanzia Leo April 4-7,2024 katika Bonanza la Maadhimisho ya Siku ya Afya Duniani yanayokwenda sambamba na Kaulimbiu isemayo"Afya Yangu,Haki Yangu".
Bonanza linafanyika katika Uwanja wa CCM Kiawala Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro.
Timu zinazoshiriki ni Turiani ,Volcano, Kidudwe,Docus, Nassoro, Nyuki ,Lusanga na Kisala ambapo mechi ya leo saa nane timu zitakazocheza ni Turiani City na Volcano ikifuatiwa na mchezo kati ya Kidudwe na Docus huku huduma mbalimbali za Afya zikiendelea uwanjani hapo.




