WAZIRI JAFO AIOMBA FAO KUUNGA MKONO SERIKALI USIMAMIZI WA MAZINGIRA

MUUNGANO   MEDIA
0



 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt.

Selemani Jafo ameliomba Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO)

kuendelea Kuunga mkono mipango ya Serikali ya Tanzania katika usimamizi

wa mazingira na kupambana na athari za mabadilko ya Tabianchi.

Pia, ameolimba shirika hilo kuisaidia Tanzania kitekenolojia, ubunifu, mafunzo

na masuala ya kifedha kwa miradi ya maendeleo, katika Sekta ya Kilimo,

Mifugo na Uvuvi hususan Ajenda 10/30.

Ametoa ombi hilo alipokutana na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa FAO Bi. Maria

Helena Semedo katika Mkutano wa Uwili jijini Nairobi nchini Kenya wakati wa

Mkutano wa Sita wa Baraza wa Mazingira Duniani (UNEA6).

Katika kikao hicho kilicholenga kuimarisha uhusiano baina ya Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania na FAO, Dkt. Jafo amelishukuru kwa kazi kubwa

wanayofanya nchini tangu Tanzania ijiunge na shirikia hilo mwaka 1962 na

tangu shirika hilo lilipofungua Ofisi zake nchini mwaka 1977.

Ameongeza kuwa FAO imekuwa ikishirikiana vyema na Tanzania katika

kujengea uwezo wataalamu wa Serikali, kusaidia katika usalama wa chakula

sambamba na sekta ya Kilimo, Mazingira na masuala mbalimbali ya

kimaendeleo.

Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi Mkuu Bi. Semedo amemuhakikisha

Waziri Dkt. Jafo na Serikali ya Tanzania kwamba FAO itaendelea kudumisha

ushirikiano wao kwa kuweka nguvu katika sekta ya Mazingira.

Halikadhalika ameihakikishia Tanzania kuwa shirika litaendeleza utekelezaji wa

mipango mbalimbali ya maendeleo hususan kuongeza tija katika kilimo ili

Tanzania iweze kufikia malengo iliyojiwekea.

Itakumbukwa kuwa Mkutano UNEA6 huo uliofanyika Februari 26 hadi MNachi

mosi, 2024 ulichagizwa na kaulimbiu 'Juhudi Madhubuti, Jumuishi na Endelevu

za Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi, Uharibifu wa Bioanuai na Uchafuzi‘.

Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Waziri Dkt. Jafo akiambatana na Naibu

Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan

Mitawi pamoja na wataalamu kutoka Ofisi hiyo.

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)