WANAWAKE NCHINI WAMETAKIWA KUTAMBUA MATUMIZI SAHIHI YA FEDHA ILI WAJIKWAMUE KIUCHUMI.

MUUNGANO   MEDIA
0


WANAWAKE Nchini wametakiwa kutambua swala la matumizi sahihi ya fedha Ili kuweza kujiongezea kipato zaidi na kujikwamua kiuchumi.


Hayo yameelezwa na  Mkurugezi Msaidizi sehemu ya usimamizi Rasilimali watu Wizara ya fedha Bi, Faudhia Nombo wakati akimwakilisha katibu mkuu wizara ya fedha Katika  maonesho ya Banda la wizara hiyo  Leo Tarehe 7 march siku ya ufunguzi  wa maonyesho ya wanawake  kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.


Amesema wizara inaendelea kutoa Elimu kwa wanawake kujiandaa wakati wa kustafu kazi Katika kipindi Cha uzeeni pamoja na swala la kutunza fedha 


" wizara haitokaa kimya ila itahakikisha inaendelea kutoa Elimu kwa wanawake ili pindi wanapostafu kazi wapate fedha za kujikimu kipindi  Cha uzeeni , wapo wanawake wanatumia fedha Katika majukumu ambayo Si sahihi na mwisho wa siku fedha ipotea na kuwa na mwisho mbaya uzeeni" amesema Nombo.


Aidha amesema kuwa wanawake wengi wanatamani kuingia Katika vikoba Ili kuweza kujikimu kiuchumi ila wanashidwa kutambua namna ya utunzaji wa fedha hivyo wizara imeona watoe mafunzo ya namna ya kutunza fedha Katika maonesho ya siku ya wanawake Dunia.


Pia ametoa wito kwa wanawake wa Dodoma kutambua Fursa zilizopo Katika wizara hiyo na kutumia kiusahihi Ili kufanikisha shughuli Zao za kiuchumi. 

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)