UBADHIRIFU NHIF; 148 WACHUKULIWA HATUA, 129 NI WATUMISHI VITUO BINAFSI

MUUNGANO   MEDIA
0

 UBADHIRIFU NHIF; 148 WACHUKULIWA HATUA, 129 NI WATUMISHI VITUO BINAFSI



Meneja wa Kitengo cha Kupambana na Udanganyifu kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ( NHIF) Bi. Rose Ntundu   ametoa ufafanuzi dhidi ya taarifa za upotoshaji zinazosambazwa mtandaoni kuhusu watumishi 148 wa NHIF kuhusika kwenye vitendo vya udanganyifu.

Bi. Ntundu  ametoa ufafanuzi huo Jijini Dar Es Salaam wakati akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari ambapo amesema kuwa kwenye taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali( CAG) iliyotolewa Machi 2023 ilieleza kuwa kati ya watumishi 148 walibainika wamehusika kwenye vitendo vya udanganyifu, watumishi 129 walitoka kwenye Vituo binafsi vya kutolea huduma huku watumishi 19 pekee walitoka NHIF.

Amebainisha kuwa tayari hatua za kisheria na nidhamu zimechukuliwa kwa watu hao kupitia mamlaka zao za ajira, bodi au mabaraza ya kitaaluma huku kwa watumishi wa NHIF waliohusika wote tayari wamechukuliwa hatua. 

“Nichukue fursa hii kuwasihi wanachama wetu, watoa huduma na waajiri kujiepusha na vitendo vya udanganyifu, Mfuko utachukua hatua kwa mtu yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo vya udanganyifu”


 amesisitiza Bi. Ntundu.

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)