MZUMBE YAWAFARIJI WAATHIRIKA WA MAFURIKO KILOSA

MUUNGANO   MEDIA
0


Chuo Kikuu Mzumbe katika kuadhimisha Siku ya Wanawake duniani Machi 6, 2024

kimetoa msaada kwa waathirika wa mafuriko katika Wilaya ya Kilosa wenye thamani

ya Shilingi 4,135,000/-

Akiwasilisha msaada huo, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Allen Mushi

amesema Mzumbe ina utamaduni wa kugusa jamii kila Maadhimisho ya Siku ya

Wanawake Duniani ambapo kwa mwaka huu msaada uliotolewa umekuwa

mahususi kwa kaya zilizokumbwa na mafuriko hapa wilayani Kilosa.

“Tumeleta  sare za shule kwa watoto wa kike na kiume, madaftari, kalamu na

penseli, miswaki na dawa za meno. Vifaa vingine ni pamoja na sabuni za kufulia,

taulo za kike na chumvi.” Prof. Mushi aliweka bayana. 

Aidha, amesema kuwa kwa muda wa siku tatu Chuo Kikuu Mzumbe kupitia Kituo

cha Msaada wa Kisheria kutoka Kitivo cha Sheria kimeendelea kutoa huduma za

kisheria bure katika  masuala ya mirathi, ardhi, ndoa na masuala mtambuka wilayani

hapo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Akipokea misaada hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Shaka Hamdu Shaka

ameushukuru uongozi na timu ya wawakilishi kutoka Chuo Kikuu Mzumbe kwa

msaada huo na kusisitiza kuwa Wilaya hiyo imekumbwa na mafuriko makubwa toka

mwezi Desemba 2023.

“Ninakuhakikishieni  kwamba msaada huu utawafikia walengwa na tunakupongezeni

sana kwa kutoa msaada wa kisheria kwa siku tatu wilayani kwetu, mwitikio ni

mkubwa na ninashauri tuweke utaratibu endelevu wa kusogeza huduma hii kwa

wananchi walau huduma hii iwe inatolewa kila mwezi” Amesisitiza Mhe. Shaka. 

Amesema Chuo Kikuu Mzumbe kimechagua mahali sahihi kutoa huduma ya kisheria

kwa kuwa Kilosa ni wilaya yenye migogoro mingi ya ardhi, ndoa na mirathi; hivyo,

msaada huo ni vema ukawa endelevu ili kutatua changamoto zinazowakabili wakazi

wa wilaya hiyo.

 

Haya yote yanafanyika ili kuiishi kaulimbiu ya Chuo Kikuu Mzumbe: "Tujifunze kwa

maendeleo ya watu"

 

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)