Waziri wa Afya Mhe. @ummymwalimu
leo Disemba 29, 2023 amewasili katika Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara
na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga ambapo
amewashukuru na kuwapongeza kwa huduma za Afya wanazoendelea kuzitoa.
Akiwa
Hanang Waziri Ummy Mwalimu anatarajiwa kukagua hali ya utoaji huduma za
afya katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, Vituo vya
Afya, Zahanati na kuzungumza na watumishi wa Afya.
Aidha Waziri
Ummy atatembelea Vituo vya kutolea huduma za Afya ambavyo viliathirika
na maafa ya maporomoko ya matope ambayo yalisababisha vifo vya watu
zaidi ya 80 pamoja na uharibifu wa miundombinu na mali.