Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan atoa
salamu za pole na kutoa maelekezo kwa vyombo vinavyoshughulikia maafa
yaliyotokea katika kijiji cha Katesh Wilayani Hanang Mkoani Manyara.
Ni
muhimu kila mmoja wetu kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Mvua kubwa
ikiwemo kuacha kupima nguvu ya maji, kuacha kusimama chini ya mti pindi
Mvua inaponyesha, kuzuia watoto kucheza kwenye madimbwi au karibu na
kingo za mito.
Aidha, ni muhimu kuzuia mlipuko wa Magonjwa
ikiwemo Malaria kwa kufukia madimbwi,kutumia chandarua kila unapolala
hata mchana na kusafisha Mazingira yote yanayokuzunguka.