DKT. MOLLEL AWATAKA WANANNCHI KUTOFICHA WATOTO WENYE USONJI

0

NAIBU Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel ametoa wito kwa wananchi kutowaficha watoto wenye changamoto ya Usonji (autism) kwani wakipata malezi na mafunzo mazuri watasaidia kuleta matokeo chanya katika jamii.

Dkt. Mollel amesema hayo leo Desemba 3, 2023 wakati akifungua Mkutano wa kimataifa wa Usonji (autism) uliofanyika katika kituo cha kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Ikumbukwe kuwa Usonji ni tatizo linalojitokeza mapema utotoni, ambapo mtoto huwa na mapungufu kwa kupenda kujitenga na kutotaka kuwa karibu na watu (Impaired social interaction), hupata matatizo ya lugha na shida ya mawasiliano (impaired language and communication skills) na huwa na tabia ya kurudia rudia kitu anachokifanya mara nyingi (restrictive repetitive behaviour).

Mara nyingi wazazi hugundua watoto wao wana tatizo hili katika kipindi cha miaka miwili ya umri wa mtoto.Chanzo halisi cha tatizo hili la usonji hakijulikani ingawa matatizo ya kijenetiki (Neurodevelopmental disorder) ndio uhusishwa na tatizo la usonji.Maaambukizi ya Rubella au matumizi ya pombe na madawa ya kulevya aina ya coccaine wakati wa ujauzito na hata sababu za kimazingira, yote haya uhusishwa na tatizo hili la usonji.

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)