Na Issa Mwadangala
Mtunza Hazina wa Machifu mkoa wa Songwe Chifu Sibhelwa Nzunda amemueleza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Theopista Mallya wakishirikiana kwa pamoja kwa kutoa elimu hususani ya ukatili wa kijinsia pia kukemea vitendo vyote viovu vinavyofanywa na jamii wanaweza kuzuia na kutokomeza uhalifu na ukatili na unyanyasaji dhidi ya watoto.
Chifu Nzunda aliyasema hayo Disemba 4, 2023 baada ya kamanda Mallya kumtembelea nyumbani kwake kwa lengo la kujadili mambo mbalimbali yanayotokea mkoani Songwe ili kuweza kukabiliana nayo kwa njia ya kutoa elimu kwa jamii hususani kwa watoto wadogo ili kuzuia changamoto ya mmomonyoko wa maadili na kuzilinda mila na tamaduni za Mtanzania.
Sambamba na hayo Kamanda Mallya alimuomba Chifu Nzunda kukemea vikali vitendo vya ukatili wa Kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto pamoja na uhalifu mwingine pia kukemea watu wanaowaozesha watoto wao kwa kisingizio cha umasikini kwani serikari kupitia Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt Samia Suluhu Hassan ameelekeza kuwa elimu ni bure na kaboresha miundombinu rafiki kwaajili ya kusomea kufanya hivyo kutauweka mkoa wa Songwe katika hali ya amani na usalama.