Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt.Doto Biteko leo amekagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Nishati na Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) katika Mji wa Serikali- Mtumba jijini Dodoma.
Dkt.Biteko katika ziara hiyo aliambatana na Katibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt.Jimmy Yonaz, na watendaji mbalimbali kutoka Wizara hizo mbili.
Katika Jengo la Wizara ya Nishati, Dkt. Biteko alikuta ujenzi
unaendelea ambao kwa sasa umefikia asilimia 69 ambapo Mkandarasi ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Aidha ujenzi wa jengo la Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Bunge na Uratibu), unaendelea vizuri huku ukiwa umefikia asilimia 74 na Mkandarasi ni SUMA JKT.




