Katika Picha ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokelewa na kupiga picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa FAO Dkt. Qu Dongyu alipowasili kwenye makao makuu wa shirika hilo.
Mheshimiwa Majaliwa anamuwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa Jukwaa la Kimataifa la Chakula Duniani linalofanyika kuanzia Oktoba 16, 2023 hadi Oktoba 20, 2023.