Wafanyabiashara wa Tengeru Mkoani Arusha walalamikia Viongozi wa Mamlaka mbali mbali za Serikali Wilayani humo kushindwa kutekeleza maagizo ya Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hasani yenye dhamila njema kwa wafanyabiashara hatimaye Viongozi hao wanashidwa kutimiza haja za wafanyabiashara wao.
Mmoja miongoni mwa Wafanyabiashara hao, Aloyce Mallya amebainisha uwepo wa ukosefu wa Soko katika eneo hilo, Pia hata eneo ambalo linatumika kama Soko Katika Sehemu hiyo kuwa na Miundombinu mibovu ikiwemo huduma za vyoo pamoja na barabara hali inayohatarisha Afya ya biashara, Wafanyabiashara na watumiaji wengine wa eneo hilo.
Hayo yamesemwa Leo na wafanyabiashara wa Tengeru Mkoani Arusha wakati wa Mkutano wa Viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) na Wafanyabiashara wa eneo hilo uliofanyika lengo ikiwa ni kupokea, kuchakata na kutolea ufafanuzi wa kero, changamoto na maoni ya Wafanyabiashara.
Wamesema wanashidwa kufanya biashara kutokana na ufinyu mdogo wa eneo la biashara siku za minada hivyo wanaiomba serikali kuwapa eneo ambao litatumika kufanyiwa biashara Zao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania Hamis Livembe amesema kuwa nia ya Serikali ya awamu ya Sita ni kutatua kero zote za wafanyabiashara nchini hivyo kero hizi zote tunazifikisha sehem husika kwa ajiri ya kupata ufumbuzi.
Awali Katibu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania Abdalla Salim amewataka wafanyabiashara wawe wazi kusema kero zao ili kupata ufafanuzi na ufumbuzi wa kero zao na huku akiwahimiza wafanyabiashara hao kujaza fomu ili wasajiliwe na kupata kitambulisho kwani kila Sekta duniani ina utambulisho wake. Pia kupitia Kitambulisho hicho kitawasaidia kutatuliwa changamoto Zao na Viongozi wa Jumuiya kwa kushirikiana na Mamlaka husika kutatua changamoto hizo.
Nae Katibu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Mkoa wa Tanga Ismail Masoud amesema kuwa Rais Samia anawapenda wafanyabiashara ndio maana ametoa Fursa ya kufanya mikutano Nchi nzima ili wafanyabiashara waweze kuwasilisha changamoto na kero zao
Pia Katika hatua nyingine amewasisitiza wafanyabiashara watumia Jumuiya kama chombo Cha uwasilishi na utatuzi wa kero Zao.