SHIMIWI YAWAWEKA WATUMISHI PAMOJA

MUUNGANO   MEDIA
0

 


Na. Asila Twaha, Iringa.

Mashindano ya Shirikisho la la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) imekuwa kitu kizuri cha kuwafanya watumishi kuwa kitu pamoja.


Hali hiyo imeionekana tarehe 2 Oktoba, 2023 wakati mchezo wa netiboli kati ya TAMISEMI na TARURA uliochezwa katika Chuo Kikuu cha RUAHA Njiani Iringa.


Kwa upande wa Kocha wa TARURA Zawadi Mwangosi amesema michezo ya  SHIMIWI imekua kitu kizuri sababu imefanya watumishi kuwa na kitu kimoja na kuwa karibu zaidi kwa kujuana na kubadilishana uzoefu sio tu kikazi hata kimichezo.


Amesema kama ratiba ilivyoonekana katika timu ya TARURA kuwa kundi E ambapo timu ya TAMISEMI kupangwa kundi E na kukutanishwa kucheza pamoja ambapo kikazi TARURA ipo chini ya Ofisi ya Rais -TAMISEMI kwa hali hii hawa ni watu wa baba mmoja wamepata nafasi ya kujuana zaidi kimichezo na kujifunza.


"TARURA babayao ni TAMISEMI mbali ya ushindi wa TAMISEMI walioupata  lakini pia kuna elimu tumejifunza kutoka kwa wenzetu TAMISEMI"  amesema Mwangosi.





Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)