HAKUNA KIWANDA KINACHOZALISHA DAMU, TUJITOKEZE KUCHANGIA - SERIKALI.

MUUNGANO   MEDIA
0

 


Na WMJWMM, Dodoma.

Serikali imewataka watu mbali mbali kujitokeza kwa wingi ili yakuchangia damu itakayo saidia kuokoa maisha ya watu wengine kwani hakuna kiwanda cha uzalishaji wa damu.


Pia Serikali imesema Utoaji wa damu ni thawabu na sadaka muhimu sana kwa mtu anapojitolea.


Akizungumza wakati wa Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali lililo kwenda sambamba na zoezi la afua ya uchangiaji wa damu, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Ziada Sellah amesema ni ukweli kwamba hakuna kiwanda chakuzalisha damu hivyo kila mtu lazima awiwe kuchangia kwa nafasi yale


Katika juhudi za kutatua changamoto ya uhitaji wa damu Serikali imeamua kutumia mbinu ya kuhamasisha wananchi kuchangia damu kwenye mikusanyiko ya watu ili kukabiliana na changamoto hiyo.



“Nitoe rai watu wajitokeze kwa wingi katika zoezi hili la kuchangia damu kwani wagonjwa wanapozidiwa na kuhitaji damu ni lazima wapatiwe kwa uharaka.


Wanawake wanapokwenda kujifungua wanakua katika hatihati ya kupoteza damu nyingi na uhitaji wa damu unatakiwa uwe wa papo hapo bila mjadala ili kunusuru maisha yao” amesema Ziada.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Mwantumu Mahiza amewakumbusha wananchi kuwa hakuna kiwanda kinachoweza kutengeneza damu ya binadamu hivo njia pekee ya kuvuna damu kwenye magala ya damu ni kujitokeza kujitoa kwani zoezi hilo ni sadaka.

“Kuchangia damu ni sadaka nzuri sana kwani ni suala linaloenda kunusuru maisha ya mtu anaepigania uhai.wake hivyo nawasisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi na Mwenyezi Mungu atatubariki” amesema Mahiza.


Naye Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Dodoma mapama kabala yakumkaribisha Mgeni Rasmi, Dkt. Nelson Bwairu amesema zoezi la kuchangia damu linatakiwa kuwa endelevu na siyo tu kwenye matukio kwani bado kuna uhitaji wa damu kwenye magala ya damu.


“Wananchi wengi hawajui kwamba zoezi la kuchangia damu linaweza kufanyika siku yeyote mtu anapoamua kuchangia kwani anaweza kwenda hospitali na kuchangia na si suala la mara moja, anaweza kuchangia mara nyingi awezavyo endapo ana vigezo vya kuchangia damu” amesema Bwairu.





Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)