RAIS SAMIA AIPONGEZA WIZARA YA MAJI USIMAMIZI MZURI WA FEDHA ZA MIRADI.

MUUNGANO   MEDIA
0

Na Mwandishi Wetu, Iramba-Singida.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameipongeza Wizara ya Maji kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maji na matumizi mazuri ya fedha.


Wizara ya Maji. inayoongozwa na Mhe. Jumaa Aweso (Mb) imepewa pongezi pamoja na Wataalamu wa Wizara hiyo kwa matumizi mazuri ya fedha za miradi katika utekelezaji na usimamizi mzuri  nchini,na kuagiza iwe mfano katika miradi mingine yote ya serikali.


Mhe. Rais ametoa pongezi hizo  baada ya kuridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi ya maji nchini, ikiwemo utekelezaji wa Mradi Mkubwa wa Maji unaotumia  chanzo cha Ziwa Victoria wa aTinde - Shelui aliouzindua leo Oktoba 17,2023 katika Kijiji cha Kisonzo, Shelui-Singida.


Mhe. Rais ameiagiza Wizara ya Maji kuongeza kasi katika usambazaji wa maji kwa wananchi, kwani amefarijika kuona suala la maji linafanyiwa kazi na serikali na maji yanapatikana tofauti na awali alipokuwa anapokelewa katika ziara zake na ndoo na chupa za maji wananchi wakielezea tatizo la maji, hali ambayo haipo tena.


Katika kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maji,  ameziagiza Mamlaka zinazohusika kuhakikisha hapatokei mkwamo kwa sababu zozote katika upatikanaji wa misamaha ya kodi inayostahili,ucheleweshaji wa vibali vya kazi kwa wafanyakazi wa kigeni na utoaji wa vifaa bandarini.






Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)