MRS GEORGIA KUTOKA ATLANTA ATEMBELEA BUSTANI YA WANYAMAPORI HAI MLIMANI CITY*

0

 *MRS GEORGIA KUTOKA ATLANTA ATEMBELEA BUSTANI YA WANYAMAPORI HAI MLIMANI CITY*







Na Beatus Maganja, DAR ES SALAAM

Mwanamke mashuhuri na balozi wa  Taasisi  ya Global Women Wealth Worriors Leaders iliyopo Atlanta Marekani Leo Oktoba 7, 2023 ametembelea bustani ya Wanyamapori hai iliyopo Mlimani City katika maonesho ya Saba ya Kimataifa ya Swahili International Tourism Expo (SITE) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam


Mrs Georgia ambaye ni mlimbwende na mwanamke mwenye ushawishi mkubwa katika masuala ya uongozi na biashara nchini Marekani ameeleza kufurahishwa kwake na ubora wa maandalizi ya maonesho ya SITE na kuwaona Wanyamapori hai mubashara katika maonesho haya.


Pamoja nae Mrs Georgia aliambata na timu ya wamarekani watano ambapo amewataka wamarekani wote kutembelea bara la Africa hususani Nchi ya Tanzania kwakuwa ni Nchi yenye utajiri mkubwa wa vivutio vya utalii hasa rasilimali Wanyamapori na kuahidi kuwa balozi mzuri wa vivutio vya utalii vilivyopo nchini.


Maonesho ya SITE yanatarajiwa kufikia tamati kesho Oktoba 8, 2023

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)