MKOA WA DODOMA WAPATA HATI SAFI KATIKA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2023.

0

 MKOA WA DODOMA WAPATA HATI SAFI KATIKA MBIO ZA  MWENGE WA UHURU 2023.














Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule Leo Octoba 07,2023  wakati akikabidhi Mwenge wa Uhuru 2023 kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendiga katika Viwanja vya Shule ya Msingi Dosidosi iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto. 


Mhe.Senyamule akitoa taarifa za hitimisho kwa mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 kwa Mkoa wa Dodoma, amesema Mwenge umekimbizwa kwa takribani kilometa elfu moja Mia nane na tisini na tatu (1893) na umepitia jumla ya Miradi ya kimaendeleo arobaini na tano (45) ambapo miradi kumi na mitano (15) imewekwa  mawe ya msingi, miradi kumi na tisa (19) imezinduliwa  na kumi na moja (11) imetembelewa yote ikiwa na jumla ya thamani ya zaidi ya shilingi Billioni 16. Miradi hiyo ni pamoja na miradi ya sekta za elimu, afya na miradi ya utunzaji wa Mazingira.


 Aidha amesema kuwa Mwenge umepita katika Wilaya zote saba  (7) na Halmashauri  nane (8) za Mkoa wa Dodoma ambazo ni zikiwemo Bahi, Chemba, Kondoa Dc ,Kondoa Mji, Dodoma jiji , Chamwino, Mpwapwa na kumaliza mbio zake kwenye Wilaya ya Kongwa.


"Dada yangu Queen Sendiga na Viongozi wote mliokusanyika hapa nitumie fursa hii kuwatangazia na kuwajulisha kwamba, Miradi yote 45 katika Mkoa wa Dodoma imepita salama bila kukataliwa na mbio za Mwenge wa uhuru 2023, hivyo niwapongeze sana Wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka huu 2023 kwa kazi hii iliyotukuka mlioifanya Dodoma" ameeleza Senyamule 


Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, ameahidi kutekeleza maelekezo kwa sehemu zote ambazo Viongozi wa mbio za Mwenge wameshauri kufanyiwa marekebisho ambapo Mkoa utahakikisha maeneo hayo yanaboreshwa.


Kwa Upande Wake, Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendiga wakati akipokea Mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Senyamule, amesema mwenge wa Uhuru utakapo kuwa Mkoani mwaka,  utatembelea miradi ipatayo 57 yenye thamani ya jumla ya shilingi Billioni 13.2, utaweka mawe ya msingi, utazindua na kukagua miradi mbalimbali. 


Nae, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Taifa  Bw.Abdalla Shaib Kaim ameupongeza Mkoa wa Dodoma kwa kupata hati safi katika miradi yote iliyokaguliwa na Mwenge wa uhuru huku akifurahishwa na  ushirikiano ulioonyeshwa na Viongozi katika kitika Kipindi chote Mwenge ulipokua ndani ya Mkoa huo.

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)