Mbunge viti Maalum Tasks Mbogo akihesabu fedha ili amkabidhi Mwenyekiti wa Chama Cha Mapindu CCC wilaya ya Mlele kwaajili ya kununua bati bando 8 .Picha na Mary Baiskeli.
Makabidhiano ya fedha hizo baina ya Mbunge Viti Maalum Taska Mbogo na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mlele Walfgang Pinda.Picha na Mary Baiskeli.
Viongozi wa chama na wanachama wa CCM wilaya ya Mlele wakiwa na Mbunge wa viti Maalum Taska Mbogo eneo la mradi.Picha na Mary Baiskeli.
Na Mary Baiskeli, Katavi.
Mbunge wa Viti Maalum kupitia Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania UWT mkoa wa Katavi Taska Mbogo amechangia shilingi milioni 3 kwaajili ya ujenzi wa ofisi za Makao Makuu ya Chama chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Mlele.
Mhe Mbogo baada ya kutembelea eneo la mradi huo ameridhishwa na utekelezaji wake na kuamua kuchangia fedha hizo taslimu ikiwa ni moja ya kuunga mkono jitihada za chama na wanachama kukamilisha ujenzi huo.
“Niwiwa kuchangia fedha hizi kwa mchanganuo ufuatao zitanunuliwa bando nane za bati kati yake nne zitapelekwa kwenye mradi wa ujenzi ofisi ya UWT,”
“Watu wamejitolea michango yao kwakushirikiana na wadau ni jambo jema sana watapata sehemu sahihi ya kufanyia shughuli za chama,”amesema Taska.
Awali Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Mlele Joshua Mbwana amesema jengo hilo litakuwa na ofisi zaidi ya tano na litaleta tija kwa wanachama baada ya kukamilika.
“Kutakuwa na ofisi ya Mwenyekiti,Katibu, Wabunge na Makatibu wao, wenyeviti wa Jumuiya zote, ukumbi na vibanda vya maduka 50 ili kuongeza uchumi,”
“Ofisi tunayotumia ni ndogo tukihitaji kufanya kikao watu zaidi ya watu kumi na tano lazima tutafute sehemu nyingine,kufanya vikao vya chama nje siyo vizuri sana,”amesema Mbwana.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Mlele Wofgang Pinda baada ya kukabidhiwa fedha hizo amesisitiza zitumike ipasavyo.
“Undeni kamati ya ujenzi sitaki kusikia hela haijulikani ilipomimi ni mkorofi kweli kwasababu huyu mama kaamua kutuchangia angeleka kwake nani angemuuliza?,”amesema Pinda.
“Amekuja kutusaidia isitokee mtu adhani ndiyo kapata fedha ya kufanya biashara kwa hiyo ni marufuku sitarajii kusikia mambo tofauti,”
Nao baadhi ya wanancha wakiwemo UWT wamepongeza hatua ya Mbunge huyo kujitoa kuchangia fedha hizo wakiwaomba na Wabunge wengine kuiga mfano huo.
“Hatuna cha kumlipa Mungu ndiyo anajua ametosaidia vitu vingi sana ikiwemo usafiri, matofali kwaajili ya ujenzi ofisi ya UWT ameonesha upendo na uzalendo,”amesema Maria Mchomvi.
Mradi huo upo hatua ya lenta umeanza kutekelezwa February 2022 ukitarajiwa kukamilika Desemba 2024 utakamilika utakaogharimu zaidi ya shilingi milioni 280.