Katikati ni Mbunge wa Jimbo la Katavi Izack Kamwelwe akimkabidhi majiko ya gesi kwa baadhi ya watumishi Idara ya elimu na afya Halmashauri ya wilaya ya Mlele.
Baadhi ya watumishi wa Idara ya elimu na afya waliogawiwa majiko ya gesi.
Watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Mlele wakiwemo Wakuu wa shule za Sekondari,Walimu wauu shule za msingi na Waganga Wafawidhi zahanati,vituo vya afya na hospitali wakishukru kupata majiko hayo.
Na Mary Baiskeli Katavi.
Mbunge wa Jimbo la Katavi Izack Kamwelwe amekabidhi majiko ya gesi 100 kwa wakazi na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Mlele iliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan ikiwa ni utekelezaji wa sera ya utunzaji mazingira.
Kabla ya kukabidhi majiko hayo ya gesi Mbunge wa Jimbo la Katavi Izack Kamwelwe amesema kufanya hivyo ni moja ya mikakati ya kuihamasisha jamii kutumia nishati mbadala ili kutunza mazingira.
“Tumeona ni faida kubwa kuchimba gesi chini ya ardhi itumike kwenye nishati badala ya kukata miti kwasababu kuna athari nyingi zaweza kujitokeza,”
“Mhe.Rais aliamua kila Mbunge akampa majiko 100 akasema nendeni mkawagawie wananchi nimeshawagawia nikaona pia shule, zahanati na vituo vya afya wapate,”amesema Kamwelwe.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mlele Soud Mbogo amemshukru rais kwa hatua hiyo kwakuwa majiko hayo yatasaidia kumtua mama mzigo wa kuni kichwani.
“Tunakushukru sana pamoja na rais ni mambo mengi anafanya katika utekelezaji wa sera na ilani tufikishie salaam zetu kwakutujali Wanamlele,’amesema Mbogo.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Mlele Teresia Irafai amesema majiko hayo ya gesi yaliyotolewa kwenye vituo vya kutolea huduma yatasaidia kiutendaji.
“Tunaishukru serikali majiko haya yatasaidia sana kwenye vituo hivi tulivyofungua kwaajili ya shughuli za kitabibu,”
Nao baadhi ya watumishi wanufaika wa majiko hayo ya gesi Wakuu wa shule za sekondari, walimu wakuu shule za msingi na Waganga Wafawidhi zahanati na vituo vya afya wamesema yatarahisisha utendaji kazi wao.
“Sisi kama idara ya afya gesi ina matumizi mengi sana kwaajili ya kutakasa vifaa vyetu ili kupunguza hali ya maambukizi kutoka kwa mtoa huduma na mteja pia hivyo tunaishukru serikali,”amesema Gilish John Mganga Mfawidhi kituo cha afya Inyonga.
Majiko hayo ya gesi 100 kati yake 56 yamegawiwa kwenye taasisi za umma ikiwemo shule, zahanati, vituo vya kutolea huduma za afya na hospitali.