WAANDISHI WA HABARI KATAVI WAPIGWA MSASA KUHUSU CHANJO YA POLIO.

MUUNGANO   MEDIA
0

 

Uploading: 692159 of 692159 bytes uploaded.


Waandishi wa Habari Mkoa wa Katavi wakiwa katika Picha ya Pamoja na watalamu kutoka Wizara ya Afya baada ya Kupatiwa Mafunzo ya Siku moja kuhusu Chanjo ya Polia.


Na Paul Mathias,Katavi.

WAANDISHI  wa habari mkoa wa Katavi wameobwa kwenda kuwa Mabalozi wazuri kwa kuelimisha jamii kwa ufasha kuhusiana na Kampeni ya Chanjo ya Polia inayotalajia kuanza Tarehe 21 hadi 24 September Mwaka kwa mkoa wa Katavi kwa watoto waliochini ya umri wa Miaka 8.

Waandishi wa Habari Mkoa wa Katavi wakiwa katika semina ya siku moja ya kujengewa uelewa kuhusu Chganjo ya Polio.

Waandishi wa habari mkoa wa Katavi wameobwa kwenda kuwa Mabalozi wazuri kwa kuelimisha jamii kwa ufasha kuhusiana na Kampeni ya Chanjo ya Polia inayotalajia kuanza Tarehe 21 hadi 24 September Mwaka kwa mkoa wa Katavi kwa watoto waliochini ya Miaka 8.

Akifunga Mafunzo ya Siku moja kwa waandishi wa Habari Mkoa wa Katavi katika kuelekea Kampeni hiyo ya Chanjo ya Polio Catherine Gitige Mratibu wa Elimu kwa Umma na ushirikishaji jamii wakati wa Dharula kutoka Wizara ya Afya amesema kuwa jamii kwa ujumla lazima izingatie kanuni bora za afya ikiwemo usafi hali ambayo itasaidia kuepukana na magojwa kama vile Polio.


''Pamoja na kwamba tunaenda Kuhamasisha Chanjo ya Polio naomba sana msisitizo uwe kwenye Kanuni Bora za Afya ni Msingi wa kwanza Kabisa kuzuia Ugojwa wa Polio  kanuni Bora za Afya usafi kwenye mazingira ,usafi wa Maji ,usafi wa vyakula tunavyokula ukienda Msalani unawe,Ukila tunda unawe,tuendelee kuwakumbusha wananchi wetu kupitia habari kwenye vyombo vyenu vya habari’’amesema Catherine.

Mratibu wa Chanjo Mkoa wa Katavi,Stephano Kahindi akitoa semina kwa waandishi wa Habari Mkoa wa Katavi juu ya umuhimu wa Chanjo ya Polio.

katika hatua nyingine amewaasa waandishi wa Habari kwenda kuibadilisha mtizamo wa Jamii juuu ya Masuala mbalimbali ikiwemo iwemo chanjo.


''Naomba sana wanaha habari mtusaidie kuelimisha kwenye Mila Potofu kuna baadhi ya jamii inaamini katika Mambo fulani fulani mtusaidie kutoa elimu kwa wananchi’'anasema Catherine.


Stephano kahidi Mratibu wa Chanjo Mkoa wa Katavi amesema kuwa Mkoa wa Katavi umejiwekea lengo la kuwafikia Watoto 2, 27862 wenye Umri chini ya Miaka 8 kwa mkoa wa Katavi.


''Tumejiwekea lengo la kuwapatia Chanjo ya Polio Watoto 2,27862 Mkoa mzima wa Katavi,Manispaa ya Manda tutachanja watoto 44,289,Halmashauri ya Nsimbo 55,429,Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika 72,373,Halmashauri ya Mpimbwe 41,813 na halmashauri ya Mlele 13,958 amesema Kahindi wakati wa Semina hiyo na waandishi wa habari mkoa wa Katavi.

Kahindi amesema kuwa chanjo hiyo itatolewa kwa njia mbalimbali ikiwemo Nyumba kwa Nyumba pamoja na kupita maeneo yenye mikusanyiko ikiwemo Masoko ili kuhskikisha Watoto wengi zaidi wanapatiwa chanjo hiyo.

Bahati Mwailafu Mwakilishi wa Kutoka Wizara ya Afya amesema kuwa wamefanya semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari Mkoa wa Katavi ili wakatoe elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa Chanjo ya Polio kwa watoto chini ya umri wa miaka 8.


Mwenyekiti wa Umoja wa Klabu ya waandishi wa Habari mkoa wa Katavi Walter Mguluchuma wakati akitoa salamu kwa niaba ya waandishi wa habari mkoa wa Katavi amesema mafunzo hayo yawe chachu kwa waandishi wa habari mkoa wa Katavi kwenda kuihamasisha jamii kupitia kalamu zao juu ya umuhimu wa kushiriki katika kampeni ya Chanjo ya Polio kwa watoto.

''Tunaishuru Wizara ya Afya na Ofisi ya Mganga Mkuu Mkoa wa Katavi kwa kupatiwa mafunzo haya ya Siku Moja kuhusu Chanjo ya Polio naimani waandishi watakwenda kuhamsisha jamii kushiriki kwenye kampeni hii kikamilifu kupitia vyombo vyao vya habari ''amesema Walter.

Kampeni ya Chanjo ya Polio itafanyika kwa Mikoa 6 Hapa Nchini kuanzia 21/9/2023 hadi 24/9/2023 kwa mikoa ya Katavi,Rukwa,Kigoma,Songwe,Mbeya na Kagera.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)