SAVE THE CHILDREN MKOMBOZI KATIKA MASUALA YA DHARURA NA MAENDELEO.

MUUNGANO   MEDIA
0

Shirika la Save the Children limekuwa na Mchango mkubwa katika Masuala ya dharura na maendeleo Kwa kushirikiana na Wadau wengine ikiwemo Shirika la Afya Duniani (WHO).


Hayo yamebainishwa Wilayani Sumbawanga Mkoani Rukwa na Mwakilishi wa Save the Children George Sungwa katika Uzinduzi wa Kampeni  ya Matone ya Chanjo ya Polio  Kitaifa kwa watoto wenye Umri chini ya miaka 8 kwa Mikoa Sita ya Rukwa, Mbeya, Katavi, Kagera, Mbeya na Songwe.


"Takriban miaka 35 ambayo tumekuwepo nchini tumefanya shughuli mbalimbali ikiwemo dharura ya mlipuko wa Magonjwa, njaa, na mambo mengine mengi" amesema.


Halikadhalika Sungwa amesema Save the Children imejikita katika mambo makuu matano ikiwemo ufuatiliaji wa Magonjwa, kumhudumia Wakimbizi, na Usalama wa chakula ikiwemo lishe.

Sungwa amesema katika kipindi cha miaka 35 Save the Children imeweza  kusaidia katika  Masuala ya dharura ikiwemo kukabiliana na mlipuko wa Magonjwa ikiwemo Uviko-19.


"Save the Children imebaki kuwa na lengo kubwa ikiwemo kuimarisha Maandalizi kabla ya dharura na jitihada za dhati Kwa kushirikiana na Wadau kama UNICEF, WHO na wengine" amesema.


Sungwa ameendelea kusema mara baada ya kuripotiwa ugonjwa wa Polio Mkoani Rukwa Save the Children ilikuja mara moja kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais TAMISEMI na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.


Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa RukwaMhe. Charles Makongoro Nyerere amelipongeza Shirika la Save the Children kwa kuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na Serikali.















Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)