RAIS SAMIA KUFUNGUA HOSPITALI YA RUFAA LINDI.

MUUNGANO   MEDIA
0

Rais  wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kesho tarehe 19 Septemba 2023 anatarajia kufungua Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi. 


Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel wakati akisalimia wananchi wa Mtama Mkoani Lindi wakati wa ziara ya Rais Mkoani humo.


Dkt. Mollel ameeleza kuwa hospitali hiyo ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi baada ya kufunguliwa itaanza  kutoa rasmi huduma  za wagonjwa wa nje (OPD), Huduma za wagonjwa wa dharura (EMD), huduma za Radiolojia na  itamaliza Rufaa zote za huduma za CT Scan  baada ya kuanza kutolewa mkoani Lindi hivyo kuwarahisishia wananchi kutosafiri kwenda Dar es Salaam na Mikoa mingine ya jirani.






Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)