Ujumbe huo wa watu watatu uliongozwa na Mshauri wa masuala ya Siasa na Uchumi katika Ubalozi huo, Bwana Jonathan Howard aliyeambatana na Bwana Andy Allen na Bi. Beatrice.
Katika mazungumzo yao Ujumbe huo ulipata fursa ya kuifahamu zaidi Tume na majukumu yake na Mpango Kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu.
Pia, katika mazungumzo yao viongozi hao walijadili maeneo mbalimbali ya mashirikiano kwa lengo la kukuza na kulinda haki za binadamu nchini.
Mkurugenzi wa Malalamiko na Uchunguzi, Bi. Suzana Pascal aliambatana na Mhe. Mwenyekiti wa Tume katika mazungumzo hayo.



