Tuzo hizi zimetolewa leo Tarehe 15 Julai, 2023 Jijini Dar Es Salaam na kupokelewa na Mwakilishi wa Katiku Mkuu Dkt. Omary Ubuguyu Mkurugenzi Msaidizi Programu ya Kudhibiti Magonjwa yasiyoambukiza pamoja Bw. Englibert Kayombo Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalino, Wizara ya Afya.
Shukrani ziwaendee waandaji wa tuzo hizi Digital Award, Viongozi wetu wakiongozwa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu kwa uongozi hodari na kuzingatia umuhimu wa nyezo za kidigitali kuweza kufikisha habari na mawasiliano kwa umma, kutumia nyezo za kidigitali kuweza kurahisisha utoaji wa huduma za afya, Taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Afya, Mabaraza na Hospitali za Rufaa za Mikoa, Waandishi wa habari na wananchi wote kwa kuendelea kufuatilia taarifa mbalimbali za Wizara kwenye mitandao yetu.