Na. Mwandishi Wetu, OR- TAMISEMI, Njombe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewekeza katika Huduma za dharura(EMD) 80 na Huduma za wagonjwa maututi (ICU) 28 katika afya ya msingi na zimekamilika zinatoa Huduma kwa wananchi.
Kauli hiyo imebainishwa na Naibu Katibu Mkuu, OfisI ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dkt. Charles Mahera wakati akizungumza na watumishi wa sekta ya afya katika mkoa wa Njombe.
Dkt. Mahera Amesema kuwa Jengo la wagonjwa wa dharura katika Hospitali ya Wilaya Makete ni miongoni mwa majengo 80 yaliyojengwa chini ya uwekezaji wa Dkt. Samia
Dkt. Mahera Amesema kuwa Dkt. Samia anaendelea kuboresha sekta ya afya ambapo hivi karibuni magari 316 ya kubeba wagonjwa yatasambazwa katika afya ya msingi ili kutoa Huduma bora kwa wananchi pale kunapotokea rufaa ya haraka.
Aidha, amewataka maafisa ustawi wa jamii na lishe kutoa elimu juu ya makuzi ya watoto kwa kuzingatia utamaduni,miongozo pamoja na elimu ya lishe ili kuondoa udumavu katika maeneo yao ya kazi.
Lakini pia, Dkt. Mahera amewataka maafisa afya nchini kuota elimu na kufanya kazi kwa weledi ili kuzuia magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.
"Maafisa wa afya fanyeni kazi yenu vizuri kwa kutoa elimu kwa ajili ya kuzuia magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu na kadhalika, tutoe elimu kwa wananchi tusiwaache wenyewe’, ameeleza Dkt. Mahera.
Dkt. Mahera amesisitiza ushirikiano kati ya hospital za rufaa, zahanati na vituo vya afya katika kutoa huduma bora kwa wananchi kwani zote ziko katika sekta moja na zinafanya kazi kwa pamoja.
"Hivi sasa vifaa vingi serikali imewekeza katika ngazi ya msingi hivyo ni wakati wa kushirikiana Hospitali za mikoa kuwajengea uwezo watumishi wa ngazi ya msingi ili vifaa vilivyowekezwa kuleta tija kwa kutoa Huduma kwa wananchi”, Amesema Dkt. Mahera.
Hata hivyo Dkt. Mahera amesisitiza Hospitali za Wilaya,vituo vya afya na zahanati kuwa na utamaduni wa kufanya ukaguzi wa dawa, vifaa tiba na ubora wa Huduma ili kubaini matumizi sahihi ya uwekezaji uliofanyika katika maeneo hayo.
Dkt. Mahera ameelekeza Waganga Wakuu wa Wilaya nchini kusimamia kwa karibu waratibu Programu kama Mfuko wa kimataifa (Global Fund) na kuhakikisha fedha za program hizo zinatumika kama zilivyopangwa na kwa wakati ili kuleta tija kwa wananchi.